Pata taarifa kuu
BURUNDI-MAUAJI-USALAMA

Milio ya risasi na milipuko ya guruneti vyasikika Bujumbura

Milio ya risasi na milipiko ya guruneti vimesikika usiku kucha, Jumapili kuamkia Jumatatu Novemba 16 katika mji mkuu wa Burundi, Bujumbura. Maeneo karibu yote ya mji wa Bujumbura yalikumbwa na hali hiyo usiku kucha, ikiwa ni pamoja na Buyenzi, Bwiza, Kinindo, Kabondo, Kanyosha, Kiriri na Musaga.

Polisi katika mitaa ya Musaga, jijini Bujumbura, mji mkuu wa Burundi, Julai 24 2015.
Polisi katika mitaa ya Musaga, jijini Bujumbura, mji mkuu wa Burundi, Julai 24 2015. REUTERS/Mike Hutchings
Matangazo ya kibiashara

Wilayani Bwiza, watu 4 ndio wamejulikana kuwa wameuawa katika mashambulizi ya Jumapili kuamkia leo Jumatatu. Inaarifiwa kuwa watu hao waliuawa katika baa moja inayopatikana kwenye njia panda kati ya barabara ya 9 na ya 5.

Msemaji wa polisi Pierre Nkurikiye, amesema askari polisi mmoja ameuawa katika mashambulizi hayo. Lakini mashahidi wamesema zaidi ya askari polisi ishirini wanasadikiwa kuuwawa katika mashambuizi hayo.

Jumatatu mchana guruneti mbili zimelipuka wilayani Buyenzi na kuwajeruhi watu kadhaa, huku milio ya risasi na milipuko ya guruneti ikisikika Jumatatu hii mchana katika eneo la Gare du Nord wilayani Kamenge, kaskazini mwa jiji la Bujumbura.

Habari ambazo hazijathibitishwa zinasema kuwa mkuu wa jiji la Bujumbura ameshambuliwa na watu waliokua wakibebelea silaha wasiojulikana. Gari moja na sehemu moja ya nyumba viliharibika kufuatia shambulio hilo. Roketi moja iliyofubaa iliokotwa karibu na nyumba anakokaa mkuu huyo wa jiji la Bujumbura.

Hali ya wasiwasi imetanda katika mji wa Bujumbura, kufuatia mashambulizi hayo, huku watu wengi wakijiuliza lini hali hii itakomeshwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.