Pata taarifa kuu
TUNISIA-SHAMBULIZI-USALAMA

Tunisia: watu wasiopungua 14 wauawa katika mashambulizi dhidi ya basi la walinzi wa rais

Watu wasiopungua 14 wameuawa Jumanne hii Novemba 24 katika mlipuko dhidi ya basi la usalama wa rais katikati mwa mji wa Tunis, msemaji wa Ikulu ya rais amesema, akithibitisha kuwa ni "shambulizi ".

VIkosi vya usalama vya Tunisia, Machi 19 jijini Tunis.
VIkosi vya usalama vya Tunisia, Machi 19 jijini Tunis. AFP/AFP/Archives
Matangazo ya kibiashara

"Watu kumi na wanne wamepoteza maisha na 11 wamejeruhiwa" katika mlipuko ambao umetokea Jumanne hii alasiri karibu na moja ya meneo makuu ya mji mkuu, Moez Sinaoui, ameliambia shirika la habari la Ufaransa la AFP.

"Ninathibitisha mlipuko ndani ya basi la usalama wa rais kuwa ni shambulizi", ameongeza msemaji wa Ikulu ya rais nchini Tunisia.

Msemaji wa wizara ya mambo ya ndani, Walid Louguini, awali alibaini kwenye kanda ya kwanza ya runinga ya serikali kuwa watu 11 walipoteza maisha.

Rais wa Tunisia Beji Caid Essebsi ametangaza hali ya hatari nchini kote Tunisia kwa muda wa siku 30 na amri ya kutotoka nje katika mji wa Grand Tunis. Mkutano wa Baraza la Usalama la Kitaifa unapangwa kufanyika Jumatano hii asubuhi.

Mwandishi wa habari wa shirika la habari la Ufaransa la AFP ameweza kuona sehemu moja ya basi ikiteketea kwa moto karibu na mtaa wa Mohamed wa 5, karibu na eneo lililofungwa. Magari mengi ya wagonjwa, maafisa wa Zima moto na vikosi vya usalama walikua katika eneo la tukio, kwa mujibu wa chanzo hicho. Watu wengi machozi yalikua yakiwatiririka.

"Maafisa wengi ambao walikua ndani ya basi wamefariki", chanzo cha usalama kilio kwenye eneo la tukio kimesema.

Wizara ya mambo ndani haikuweza kutaja ni watu wa ngapi ambao walikua ndani ya basi hilo.

Tunisia ilikabiliwa na mashambulizi kadhaa ya kijihadi mwaka jana, ambapo mashambulizi mawili dhidi ya makavazi ya Bardo mjini Tunis mwezi Machi na dhidi ya hoteli moja karibu na mji wa Sousse mwishoni mwa mwezi Juni, yaliwaua watu 60.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.