Pata taarifa kuu
TUNISIA-SHAMBULIO-UGAIDI-USALAMA

Tunisia: watu 37 wauawa katika shambulio

Watu 37 wameuawa na wengine zaidi ya 36 wamejeruhiwa Ijuma wiki hii katika shambulio la risasi katika eneo la utalii la Sousse, katikati mwa Tunisia. Mshambuliaji mmoja ameuawa, kwa mujibu wa viongozi.

Raia kutoka Uingereza, Ujerumani na Ubelgiji ni miongoni mwa waathirika wa mashambulizi dhidi ya hoteli katika mji wa Sousse, Ijumaa Juni 26 mwaka 2015.
Raia kutoka Uingereza, Ujerumani na Ubelgiji ni miongoni mwa waathirika wa mashambulizi dhidi ya hoteli katika mji wa Sousse, Ijumaa Juni 26 mwaka 2015. REUTERS/Amine Ben Aziza
Matangazo ya kibiashara
  • Mashambulizi hayo yalilenga hoteli ya Riu Imperial Marhaba ya bandari ya Al-Kantaoui, karibu na eneo la utalii la Sousse, mji unaopatikana kusini mwa Tunis.
  • Takriban watu 37 wameuawa, ikiwa ni pamoja na raia kutoka Ubelgiji, Uingereza na Ujerumani.
  • Mshukiwa wa mauaji hayo ameuawa. Ni mwanafunzi wa chuo kikuu asiyejulikana katika Idara ya polisi.

 Watu 37 wameuawa katika shambulio hilo, na huenda idadi hiyo ikaongezeka, kwa mujibu wa wizara ya afya ya Tunisia, zaidi ya watu 36 wamejeruhiwa.

Shambulio hilo limeendeshwa na mtu mmoja ambaye alikua akibebelea silaha, lakini aliuawa baada ya shambulio.

“ Kwa sasa mji wa Sousse umezingirwa na polisi ”, kiongozi wa hoteli kulikotokea mashambulio ameilezea RFI kwenye simu . Hata hivyo eneo hilo lilikua likiwekwa chini ya ulinzi mkali, kwani mwaka uliyopita, mtu aliyejitoa mhanga alijilipua, bila hata hivyo kusababisha hasara.

Rais wa Ufaransa François Hollande na mwenzake wa Tunisia Beji Caid Essebsi walionyesha "mshikamano wao dhidi ya ugaidi". Ufaransa imengwa siku kama hii na mashambulizi ya kigaidi.katika siku hiyo kutoka shambulio jingine la kigaidi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.