Pata taarifa kuu
LIBYA-SERIKALI YA UMOJA

Jumuiya ya kimataifa yatoa wito kwa serikali ya umoja Libya

Viongozi kutoka nchi ishirini na mashirika ya kimataifa waliokutana Jumapili hii katika mji Roma wametoa wito wa haraka wa kusitisha mapigano nchini Libya, na kuundwa haraka kwa serikali ya umoja ili kukomesha machafuko yanayoendelea kuikumba nchi hiyo.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry (kushoto), mwenzake wa Italia Paolo Gentiloni (katikati) na mjumbe wa Umoja wa Mataifa kwa nchi ya Libya Martin Kobler (kulia) wakihudhuria mkutano wa kimataifa kuhusu Libya, jijini Roma Desemba 13, 2015.
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry (kushoto), mwenzake wa Italia Paolo Gentiloni (katikati) na mjumbe wa Umoja wa Mataifa kwa nchi ya Libya Martin Kobler (kulia) wakihudhuria mkutano wa kimataifa kuhusu Libya, jijini Roma Desemba 13, 2015. AFP/POOL/AFP
Matangazo ya kibiashara

Serikali ya umoja wa kitaifa "inayoendesha shughuli zake mjini Tripoli iliundwa ili, kwa ushirikiano na jumuiya ya kimataifa, kukabiliana na hali inayoikumba nchi hiyo katika masuala ya kibinadamu, kiuchumi na usalama", viongozi kutoka nchi hizo wametangaza katika taarifa ya pamoja, baada ya mkutano ulioongozwa na Italia kwa ushirikiano na Marekani.

Viongozi waliosaini waraka huo wametaja hasa kundi la Islamic State (IS) "na makundi mengine yenye msimamo mkali na mashirika ya wahalifu yanayoshirikii katika aina zote za magendo na biashara, hasa ya binadamu."

"Tunatoa wito kwa pande zote kukubali kusitisha mapigano haraka na kwa jumla katika nchi nzima ya Libya", viongozi hao wameongeza, na kuthibitisha ahadi yao ya kutoa misaada ya kibinadamu. Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, watu 4.2 kwa jumla ya Walibia milioni 6 wanahitaji misaada, licha ya rasilimali za mafuta kwa kiasi kikubwa nchini humo.

Wakati ambapo wawakilishi wa makundi kadhaa ya waasi yamethibitisha nia yao ya kutia saini Jumatano katika mji wa Skhirat, nchini Morocco, makubaliano yaliyofikiwa mwezi Oktoba chini ya uangalizi wa Umoja wa Mataifa, viongozi katika mkutano huo nchini Italia wamehakikisha kwamba wataunga mkono "juhudi za raia wa Libya na kuifanya nchi hiyo kuwa sahihi, kuendelea kidemokrasia, ustawi na umoja".

"Wale wanaohusika na vurugu na wale ambao wanazuia mchakato wa amani na kudhoofisha mchakato wa mpito wa Libya watataadhibiwa kwa mujibu wa sheria", zilionya nchi 17 wanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, ikiwa ni pamoja na nchi za Ulaya na za Kiarabu, pamoja na Umoja wa Mataifa, Umoja wa Ulaya, Umoja wa Kiarabu na Umoja wa Afrika.

"Hatuwezi kuruhusu hali kama ilivyo iendelee nchini Libya" amesisitiza Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, John Kerry, wakati wa mkutano na waandishi wa habari baada ya mkutano huo. "Ni hatari kwa uwezekano wa Libya, ni hatari kwa Walibya, na wakati huu ambapo Daesh (IS) imekua ikiimarisha uwepo wake, ni hatari kwa kila mtu", amesema John Kerry.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.