Pata taarifa kuu
EU-BURUNDI-SIASA-VIKWAZO

Burundi kuchukuliwa vikwazo na EU

Baraza la Umoja wa Ulaya linakutana Jumatatu wiki hii kutathmini vikwazo ambavyo litaichukulia Burundi baada ya serikali ya nchi hii kushindwa kukomesha uhalifu unaendeshwa na maafisa wake dhidi ya raia.

Askari polisi na wanajeshi wakipiga doria katika mtaa mmoja wa mji wa Bujumbura, Februari 3, 2016, baada ya shambulio la guruneti.
Askari polisi na wanajeshi wakipiga doria katika mtaa mmoja wa mji wa Bujumbura, Februari 3, 2016, baada ya shambulio la guruneti. REUTERS/Jean Pierre Aime Harerimama
Matangazo ya kibiashara

Baada ya siku nzima ya mashauriano kati ya Burundi na Umoja wa Ulaya mjini Brussels Jumanne Desemba 8 mwaka 2015, Umoja wa Ulaya haukutoshelezwa na mapendekezo yaliyotolewa na serikali ya Bujumbura juu ya kurekebisha makosa kuhusu ukiukwaji wa haki za binadamu nchini humo.

Baada ya mashauriano hayo Umoja wa Ulaya ulitangaza kuwa utachukua hatua zinazofaa.

Wakati huo Umoja wa Ulaya ulichukua uamuzi ufuatao: misimamo "iliyotolewa na serilaki ya Bujumbura hairuhusu kurekebisha mapungufu ya ushirikiano muhimu ya Umoja wa Ulaya na Burundi". Kwa maneno mengine, serikali ya Bujumbura haikuweza kuweka wazi nia yake ya kurekebisha makosa ya ukiukaji wa haki za binadamu na misingi ya kidemokrasia ambayo inatuhumiwa.

Au hata nia yake ya kukubali haraka kuelekea katika njia ya mazungumzo ya "dhati na umoja" yanayopendekezwa na Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika.

Ni miezi kadhaa sasa Brussels ikiendelea kuongeza shinikizo kwa matumaini ya kulazimisha serikali ya Bujumbura kuanzisha mazungumzo na upinzani, bila hata hivyo mafanikio yoyote.

Hivi karibuni Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza aliwahakikishia ujumbe wa Baraza la Usalam ala Umoja wa Mataifa uliokua ziarani mjini Bujumbura kwamba serikali yake haina mpango wowote wa kuanzisha mazungumzo na upinzani ulio uhamishoni nje ya nchi, ambao aliutaja kuwa unaundwa na watu waliohusika na jaribio la mapinduzi lililotibuliwa la Mei 13, 2015.

Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, Samantha Power, pamoja na wawakilishi wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa mjini Bujumbura, Januari 22, 2016.
Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, Samantha Power, pamoja na wawakilishi wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa mjini Bujumbura, Januari 22, 2016. AFP / ONESPHORE NIBIGIRA

Bujumbura yaendelea kutengwa

Mahusiano kati ya Umoja wa Ulaya na serikali ya Bujumbura yamezorota kwa muda mrefu. Lakini kamwe katika mgogoro huu Brussels ilikua haijawahi kuonyesha msimamo wake kama inavyofanya wakati huu kutokana na serikali ya Bujumbura kutokuwa na nia ya kukomesha machafuko na ukiukwaji wa haki za binadamu pamoja na kutokubali kuanzisha mazungumzo na wadau wote wanaohusika katika kuliendeleza taifa hilo kidemokrasia. Baada ya vikwazo vya Marekani dhidi ya baadhi ya maafisa wa wa usalama na ulinzi wa Burundi, pamoja na uamuzi wa Jumuiya ya nchi za Maziwa Makuu (ICGLR) wakuondoa kwa muda makao yake makuu katika mji mkuu wa Burundi, hivyo hii ni hatua nyingine katika kutengwa kwa serikali ya Bujumbura kimataifa.

Hali ya taharuki yaendelea kutanda katika maeneo mbalimbali

Hayo yakijri, milio ya risasi na milipuko ya maguruneti vyaendelea kusikika katika maeneo mbalimbali ya Burundi, hasa katika mji mkuu wa Bujumbura. Usiku wa Jumamosi kuamkia Jumapili, ngome za jeshi zilivamiwa na kundi la watu wenye silaha katika wilaya za Ngagara na Cibitoke kaskazini mwa mji wa Bujumbura. Na usiku wa Jumapili kuamkia Jumatatu hii, milio ya risasi iliendelea kusikika usiku kucha katika baadhi ya maeneo ya mji wa Bujumbura.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.