Pata taarifa kuu
DRC-UN-WAKIMBIZI-USALAMA

DRC: mapigano yasababisha wakimbizi kutoroka kambini

Wakimbizi wa ndani kutoka kambi 5 mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo wamelazimika kutoroka kambi hizo kufuatia mapigano yaliozuka katika eneo la Mpati, mkoani Kivu Kaskazini.

Manispaa ya jiji la Bukavu, Kivu Kaskazini.
Manispaa ya jiji la Bukavu, Kivu Kaskazini. Wikimedia
Matangazo ya kibiashara

Mapigano hayo kati ya jeshi la taifa FARDC na waasi waliojihami yanaendelea kuzorotesha hali ya usalam na kusababisha wakazi wa eneo hilo na maeneo jirani kuwa na wasi wasi, huku wengi wao wakiwa wameanza kuyahama makazi yao.

Umoja wa mataifa unaohudumia kambi hizo umeeleza kwamba wakimbizi takriban 35,000 wametoroka kwa kufohia usalam wao.

Umoja wa Mataifa unasema kuwa unahofia usalama wa wakimbizi hao , ambao mpaka sasa wengi walikimbilia misituni na wengine katika maeneo jirani.

Kwa sasa ni vigumu kujua hali yao halisi kutokana na kudorora kwa hali ya usalama katika eneo Mpati mwezi mmoja sasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.