Pata taarifa kuu
SUDANI KUSINI-MACHAR-SIASA

Riek Machar aiambia RFI kuhusu kuchelewa kurudi kwake Juba

Jumuiya ya kimataifa imeonyesha wasiwasi wake Jumatano hii, kwa mchakato wa amani nchini Sudan Kusini, baada ya kiongozi wa waasi Riek Machar kuchelewa kurudi katika mji mkuu wa nchi hiyo, Juba.

Kiongozi wa waasi na Makamu wa rais wa Sudan Kusini, Riek Machar,Julai 8, 2015.
Kiongozi wa waasi na Makamu wa rais wa Sudan Kusini, Riek Machar,Julai 8, 2015. REUTERS/Thomas Mukoya
Matangazo ya kibiashara

Riek Machar anatazamiwa kuchukua majukumu yake kama Makamu wa Rais Salva Kiir atakapowasili katika mji mkuu wa nchi hiyo changa. Machar ameiambia RFI kuhusu kuahirishwa mara kadhaa kwa kurudi Juba.

Makamu wa Rais Salva Kiir, ambaye anatazamiwa kuchukua majukumu yake nchini Sudan Kusini, tayari ameahirisha mara mbili, Jumatatu 18 na Jumanne Aprili 19, kurudi kwake katika mji mkuu wa nchi hiyo, Juba, akibaini kwamba bado kuna "matatizo ya vifaa na kiutawala."

"Wameniambia kwamba tuko huru kurudi, lakini hatuna ndege itakayotusafirisha hadi Juba. Inatubidi tukodi ndege nyingine. Hali hii inaweza kuchukua siku tatu au nne, " Riek Machar ameiambia RFI.

RFI : Hii ina maana kwamba unaweza kuwa umerudi Juba hadi Jumamosi?

"Siwezi kuwajibu wakati ambapo tutakua bado hatujakodi ndege itakayofanya safari kutoka Gambella kwenda Juba na Juba-Gambela mara tatu, Machar amesema. Tutakwenda kwa gari kutoka Pagak, mji wa mpakani, hadi kwenye uwanja wa ndege wa Gambella, nchini Ethiopia. Abiria, ikiwa ni pamoja na vikosi vya kijeshi na usalama wako tayari eneo hilo, katika uwanja wa ndege wa Gambella kwa siku tatu sasa. "

Kwa upande wake, serikali ya Sudan Kusini, Jumanne hii, ilieleza sababu nyingine kuhusu kuahirishwa kurudi kwake kiongozi wa waasi, Riek Machar, ikisema kuwa masharti ya Riek Machar ya kurudi Juba na askari 200 pamoja silaha nzitonzito za ziada pamoja na makombora hayakubaliki. Jumatano hii, kiongozi wa waasi alisema kuwa amekubaliwa na serikali ya Juba kurudi.

"Sote tunataka amani"

Kurudi kwa Riek Machar kutaruhusu uundwaji wa serikali ya mpito ya umoja wa kitaifa ambayo itapelekea kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu ndani ya miezi 30 na utekelezaji wa mkataba wa amani uliosainiwa Agosti 26, 2015.

"Ni faraja kubwa, amesema Riek Machar. Tangu tuliposaini mkataba wa amani, tunahitaji kurejea Juba, ili kudumisha amani nchini kote Sudan Kusini na kuunda serikali ya umoja wa kitaifa. Tuna wizara kumi; kambi nyingine ina wizara sita; vyama vingine vya siasa vina wizara nne. Kwa upande wetu bado tunakutana kwa mashauriano ili tuweze kujaza nafasi hizo kumi. "

RFI : Na unafikiri kuwa utaweza kufanya kazi na Rais Salva Kiir?

"Mnajua hii ni serikali ya umoja wa kitaifa, tunatakiwa kufanya kazi kwa pamoja, amesema Makamu wa rais mteule. Sote tunataka amani. Kama wao hawaamini, mimi nina imani na hilo ninalozungumza! Nataka tu amani irudi, hali ya kawaida irudi katika nchi yangu. "

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.