Pata taarifa kuu
SUDANI KUSINI-MACHAR-SIASA

Mpaka sasa Riek Machar asubiriwa Juba

Kwa siku ya pili Jumanne hii, kiongozi wa waasi nchini Sudan Kusini Riek Machar hajawasili jijini Juba kama ilivyotarajiwa ili kuunda serikali ya pamoja na rais Salva Kiir.

Kiongozi wa waasi na Makamu wa rais wa Sudan kusini Riek Machar, Julai 8, 2015.
Kiongozi wa waasi na Makamu wa rais wa Sudan kusini Riek Machar, Julai 8, 2015. REUTERS/Thomas Mukoya
Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa Machar William Ezekiel amesema kutofika kwa kiongozi huyo kunatokana na serikali ya Salva Kiir kutotoa kibali cha kutua kwa ndege ya kukodi ya Machar itakayowasili pamoja na wasaidizi wake na silaha.

Inaaminiwa kuwa kwa sasa Machar yuko katika ngome yake ya Pagak Mashariki mwa nchi hiyo au Gambella nchini Ethiopia.

Hali hii imeendelea kuzua hali ya wasiwasi jijini Juba, huku kila mmoja asifahamu Machar atawasili lini.

Hat hivyo serikali ya Sudan Kusini imesema kuwa kiongozi wa waasi Riek Machar, amefutilia mbali mpango wake wa kurejea Juba kwa muda usiojulikana.

Msemaji wa serikali Michael Makuei amesema: " makamu wa Riek Machar, alitaka kurejea Juba na silaha za kivita, ikiwa ni pamoja na magari ya kivita, makombora na bunduki za kivita".

Pia Makuei amesema kuwa serikali ya Sudan Kusini imeruhusu wanajeshi1370 kati ya 1410 kurejea Juba kwa minajili ya ulinzi wa Riek Machar.

"Utawala wa Sudan Kusini hautaruhsu wanajeshi zaidi kurejeshwa Juba, kutokana na sababu za kiusalama, " amesema Michael Makuei.

Itafahamika kwamba Machar alitazamiwa kuwasili Juba tangu Jumatatu hii Aprili 18 kama ilivyokua imearifiwa siku za nyuma lakini mpaka sasa hajawasili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.