Pata taarifa kuu
SUDANI KUSINI-MACHAR-SIASA

Riek Machar aahirisha kuwasili kwake Juba

Kiongozi wa waasi nchini Sudan Kusini Riek Machar ameahirisha kuwasili kwake jijini Juba kutoka Jumatau hii hadi leo Jumanne.

Kiongozi wa waasi wa Sudan Kusini, Riek Machar, katika jimbo la  Jonglei, Sudan Kusini, Janurai 31, 2014.
Kiongozi wa waasi wa Sudan Kusini, Riek Machar, katika jimbo la Jonglei, Sudan Kusini, Janurai 31, 2014. REUTERS/Goran Tomasevic
Matangazo ya kibiashara

Msemaji wake Willima Ezekiel amesema, kuwasili huko kumeahirishwa kwa sababu kuna mambo hayajakaa vizuri.

Machar anatarajiwa kuapishwa kuwa Makamu wa kwanza wa rais kuongoza serikali ya umoja wa Kitaifa na rais Salva Kiir.

Upinzani anasema una nia ya dhati kutekeleza mkataba wa amani uliotiwa saini mwezi Agosti mwaka uliopita.

Kuundwa kwa serikali hiyo mpya kunatarajiwa kumaliza mapigano nchini humo na Katibu Mku wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amewataka viongozi wa kisiasa nchini humo kuharakisha uundwaji wa serikali hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.