Pata taarifa kuu
ETHIOPIA-USALAMA

Ethiopia: mauaji ya Gambella yaendeshwa na watu kutoka Sudan Kusini

Idadi ya watu waliouwawa katika shambulio la watu wenye silaha katika jimbo la Gambella, nchini Ethiopia, karibu na mpaka na Sudan Kusini, Ijumaa, Aprili 15, imeongezeka na kufikia 208 na watoto 102 walitekwa nyara, kwa mujibu wa Waziri Mkuu wa Ethiopia.

Jimbo la Gambella, Ethiopia, kinalopakana na Sudan Kusini.
Jimbo la Gambella, Ethiopia, kinalopakana na Sudan Kusini. © Crédit: Wikimedia Commons
Matangazo ya kibiashara

Shambulio hilo lilitekelezwa na watu wenye silaha kutoka Sudan Kusini. Inaarifiwa kuwa watu hao inaonekana walikua wamekuja kuiba ng'ombe.

Kile ambacho vyombo vya habari vya Ethiopia vimekitaja kama "mauaji ya Gambella" inaonyesha ukosefu amani katika mkoa huo wa mpaka. Tangu mwanzo wa mgogoro wa Sudan Kusini, karibu 3wakimbizi 00 000 wamekuwa waliongezeka kwa jamii ya watu kutoka makabila ya Nuer na Anouak nchini Ethiopia. Machafuko yanayoikumba Sudan Kusini yanaathiri upande wa Ethiopia.

Ethiopia kwa muda mrefu imekua ikiogopa hatari yamdororo wa usalama katika jimbo la Gambella kwa sababu ya vita nchini Sudan Kusini na Addis Ababa imewekeza sana katika mchakato wa amani.

Mara kwa mara, matukio yamekua yakizuka baina ya makabila mbalimbali na wizi wa mifugo mpakani ni kawaida.

Mashambulizi ya kipekee

Lakini shambulizi la Ijumaa lilikua kubwa tena la kipekee. Idadi ambayo bado ni ya muda inazidi watu 200 waliouawa, pamoja na zaidi ya mamia ya watoto waliotekwa nyara. Shuhuda za kwanza zinaonyesha kwamba washambuliaji ni watu kutoka kabila la Murle, hasimu wa Jamii ya watu kutoka kabila la Nuer, ambao walikua na silaha za aina ya Kalashnikovs.

jeshi la Ethiopia wamewekwa tayari na mamlaka ya Ethiopia imetupilia mali mashaka juu ya ukweli kwamba askari wa Ethiopia wanaweza hata kuwa walivuka mpaka na kuendesha operesheni katika ardhi ya Sudan Kusini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.