Pata taarifa kuu
SUDANI KUSINI-MACHAR-SIASA

Mchakato wa amani hatarini Sudan Kusini

Waangalizi wa utekelezwaji wa mkataba wa amani nchini Sudan Kusini wanaonya kuwa kutorejea kwa kiongozi wa waasi Riek Machar jijini Juba siku ya Jumatatu au jana kama ilivyotarajiwa, kunahatarisha kuzua tena kwa mapigano nchini humo.

Kiongozi wa waasi wa Sudan Kusini, Riek Machar.
Kiongozi wa waasi wa Sudan Kusini, Riek Machar. (Photo : AFP)
Matangazo ya kibiashara

Mwenyekiti wa Waangalizi hao ambaye ni rais wa zamani wa Boswtana Festus Mogae anasema, ikiwa Machar hatafika Juba hivi karibuni kuna uwezekano mkubwa wa kuanza tena kwa mapigano nchini humo na kuvunjika kabisa kwa mkataba wa uundwaji wa serikali ya pamoja, serikali ambayo Riek Machar atakuwa Makamu wa kwanza wa rais.

Wasiwasi huu pia umeonyeshwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa hatua ya kutowasili kwa Machar huku Marekani ikimshutumu kiongozi huyo wa waasi kwa kutokuwa na nia ya dhati ya kutekeleza mkataba huo uliofikiwa mwaka jana.

Lakini swali kubwa ni kwanini Machar hajarejea? Serikali ya Juba na waasi wanalaumiana kwa kutowasili Machar.

Waasi wanasema, serikali ya Juba imekataa kiongozi wao awasili. Serikali ya rais Kiir inasema wanajeshi wa waasi ambao tayari wako Juba ni 1,370 idadi ambayo serikali inasema inatosha na hivyo hakuna haja ya kuwasili kwa mamia ya wapiganaji wengine wa waasi, madai ambayo Riek Machar akizungumza na kituo cha Al Jazeera amekanusha.

Machar anasema mkataba wa amani unamruhusu kuja na wanajeshi 2,910 na yeye anataka tu kuandalama na wanajeshi 260 na anasisitiza kuwa yuko tayari kufika Juba.

Kwa hali hii, haijulikani kati ya serikali ya Juba na waasi nani anasema kweli.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.