Pata taarifa kuu
DRC-BENI-MAUAJI

Watu 17 wauawa Beni, mashariki mwa DRC

Watu wasiopungua 17 waliuawa Jumanne, Mei 3 jioni na watu wanaoaminika kuwa wapiganaji wa kundi la waasi wa Uganda la ADF katika maeneo ya Minibo na Mutsonge, vitongoji viwili vilio kwenye umbali wa kilomita takriban 60 kaskazini mwa mji wa Beni , katika mkoa wa Kivu Kaskazini.

Askari wa MONUSCO, Oktoba 23,  2014 Beni, DRC.
Askari wa MONUSCO, Oktoba 23, 2014 Beni, DRC. AFP PHOTO / ALAIN WANDIMOYI
Matangazo ya kibiashara

Vyanzo kutoka vijiji hivyo vinabaini kwamba kati ya saa 11 jioni na saa 3 usiku, washambuliaji walipenya na kuingia katika vijiji hivyo na waliwashambulia raia wakiwakuta ndani ya nyumba zao.

Vyanzo hivyo vinaarifu kuwa watu hao wenye silaha waliwashambulia raia kwa mapanga ili wasiwezi kutaarifu mapema wanajeshi na askari wa Umoja wa Mataifa wanaopiga kambi katika eneo hilo.

Msemaji wa operesheni inayojulikana kwa jina la Sokola 1, luteni Mak Hazukay, amesema watu wasiopungua 17 wakiwemo wanawake 10 na watoto 5 waliuawa katika mashambulizi hayo.

Hazukay amesema ripoti hiyo ni ya muda, na kuongeza kuwa taarifa kuhusu kuwepo kwa wapiganaji wa kundi la waasi wa Uganda la ADF katika mkoa huo imechelewa kuwafikia wanajeshi.

Kwa mujibu wa vyanzo vingine vya kijeshi, Meja Jenerali Stephen Kasereka, naibu mkuu wa majeshi anayehusika na operesheni katika Ukanda wa tatu wa ulinzi wa jeshi, amewasili Jumatano hii, Mei 4 asubuhi katika wilaya ya Baungachu-Luna, eneo ambapo kulitokea mauaji.

Afisa huyu amejielekeza katika eneo hilo ili kutathmini hali inayojiri na kuchukua hatua za kulinda raia.

"Uzembe" wa jeshi

Vyama vya kiraia katika mji wa Benivimelaani mauaji hayo na kusema watu hao waliuawa kutokana na "uzembe" kwa upande wa Majeshi ya DRC (FARDC) na askari wa MONUSCO, ambapo, kambi zao ziko mita 300 tu eneo la tukio. Kiongozi wa muungano wa vyama vya kiraia katika mji wa Beni, Teddy Kataliko, amesema kuwa raia walitoa tahadhari mapema, saa chache kabla ya mauaji hayo.

Kwa upande wake Julien Paluku, mkuu wa mkoa wa Kivu Kaskazini, ametupilia mbali tuhuma hizo. Amesema anaamini kwamba jitihada zinafanyika katika uwanja wa vita ili kulitokomeza kundi hilo la waasi wa Uganda.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.