Pata taarifa kuu
UCGLR - ANGOLA

Wakuu wa nchi za ICGLR wakutana Luanda, kujadili usalama

Mkutano wa waku wa nchi za maziwa makuu, ICGLR, umeanza rasmi mjini Luanda, Angola, ukiwa ni mkutano wa 6 kwa wakuu hao wa nchi kukutana, kwa mwaliko wa rais, Jose Eduardo dos Santos.

Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, akiwa kwenye mazungumzo na rais wa Angola, Jose Eduardo dos Santos, mjini Luanda, 14 June 2016
Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, akiwa kwenye mazungumzo na rais wa Angola, Jose Eduardo dos Santos, mjini Luanda, 14 June 2016 Kenya Govt
Matangazo ya kibiashara

Mkutano wa mwaka huu ambao umebeba dhima ya "Kuharakisha mchakato wa utekelezaji wa mikataba na itifaki kwa lengo la kujenga demokrasia na ukanda wa maziwa makuu ulio tulivu", ulitanguliwa na mkutano wa wakuu wa majeshi na mawaziri wa mambo ya kigeni, kutoka kwenye nchi hizo.

Wakuu wa majeshi na mawaziri wa ulinzi wamejadili na kuridhia ripoti mbalimbali za masuala ya usalama kuhusu nchi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati, ripoti kuhusu hali ya usalama nchini Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Sudan na Sudan Kusini.

Ripoti hizi zimewasilishwa baadaya kamati maalumu zilizokuwa zimeundwa kutathmini hali ya usalama kwenye nchi hizo, kumaliza ziara zao kwenye nchi husika ambapo waliandika ripoti ambayo itawasilishwa pia kwa wakuu wa nchi.

Masuala mengine yaliyojadiliwa na mawaziri wa mambo ya kigeni ni pamoja na kupitia ripoti ya mapendekezo kuhusu rasilimali na mali asili za nchi za ukanda wa maziwa makuu, kupokea taarifa ya mjumbe maalumu wa umoja wa Mataifa anayehusika na masuala ya amani na usalama kwenye ukanda.

Wakuu wa nchi wanaokutana Jumanne ya wiki hii, watajadili hali ya siasa kwenye nchi zao na namna bora ya kutatua mizozo ya kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu na hasa ule wa nchi ya DRC.

Mbali na masuala ya siasa, pia watazungumzia kuhusu mwenendo wa demokrasia kwenye nchi zao, hasa wakati huu ambapo baadhi ya wakuu wa nchi wakikosolewa kwenye nchi zao kwa kutaka kuminya demokrasia.

Suala la usalama ni kitu kingine ambacho kitajadiliwa kwa kina na wakuu hao wa nchi kabla ya kutangaza hatua za kuchukuliwa ili kudhibiti kutokea kwa machafuko na kuzima machafuko ambayo yanashuhudiwa kwenye baadhi ya mataifa wanachama wa ICGLR.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.