Pata taarifa kuu
RWANDA-WAKIMBIZI

Denmark kutoa hifadhi ya ukimbizi kupitia Rwanda

Ni jambo ambalo ni vigumu kuamini, lakini huo ndio uamuzi uliofikiwa na mamlaka nchini Denmark. Wageni nchini Denmark ambao wanataka kuomba hifadhi ya ukimbizi sasa watalazimika kufanya hivyo kupitia Rwanda, barani Afrika.

Maandamano ya kuunga mkono watoto wahamiaji kufuatia kisa cha moto kuzuka katika kambi ya wakimbizi ya Moria, Ugiriki, Septemba 15, 2020, huko Copenhagen.
Maandamano ya kuunga mkono watoto wahamiaji kufuatia kisa cha moto kuzuka katika kambi ya wakimbizi ya Moria, Ugiriki, Septemba 15, 2020, huko Copenhagen. AFP - EMIL HELMS
Matangazo ya kibiashara

Mfumo huu unaitwa usafirishaji wa ombi la hifadhi. Fikiria mkimbizi, mhamiaji haramu, ambaye baada ya kuvuka Bahari ya Mediterranean anajikuta nchini Denmark na anaomba hifadhi nchini humo. Atasajiliwa, kisha atawekwa kwenye ndege kwenda Rwanda, ambapo anaweza kuwasilisha ombi lake akiwa katika kituo cha wakimbizi.

Mamlaka nchini Denmark imekuwa inatafuta makubaliano na nchi kadhaa, ikiwa ni pamoja na Tunisia, Ethiopia, lakini nchi hiyo na serikali ya Rwanda zimetia zaini kwenye itifaki ya makubaliano. Mazungumzo haya yote yalifanyika kwa miezi kadhaa. Yalibaki kuwa sir, isipokuwa kwamba afisa mmoja wa Rwanda alivujisha siri hiyo baada ya kurusha kwenye Twitter picha yake akiwa na marafiki zake wapya kutoka Denmark.

Wengi wamejiuliza maswali. Je! Lengo hili ni kupunguza uhamiaji haramu? Je! Kuhusu uhamiaji? Waziri wa Uhamiaji wa Denmark Mattias Tesfaye, ambaye mwenyewe ni mtoto wa mkimbizi, amehakikisha kwamba mfumo huo utakuwa "wa kibinadamu na wa haki zaidi", kwani utapunguza wimbi la wahamiaji, ambapo watu wanahatarisha maisha yao. Lakini ni kweli kwamba lengo ni kufikiaaiwepo mhamiaji hata mmoja anasikika nchini Denmark. Ni mkimbizi gani katika mazingira haya atajaribu bahati yake kwenda Denmark?

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.