Pata taarifa kuu

Denmark yasitisha msaada kwa Mali

Wizara ya Mambo ya Nje ya Denmark imeliithibitishia shirika la habari la AFP habari iliyotolewa Ijumaa Februari 11 na gazeti la Mali L'Indépendant. Uamuzi huu unafuatia kufukuzwa kwa wanajeshi wa Denmark waliojiunga na kikosi cha Takuba nchini Mali.

Copenhagen inapenda kuendeleza miradi yake ya kibinadamu na usaidizi wake kwa mashirika ya kiraia.
Copenhagen inapenda kuendeleza miradi yake ya kibinadamu na usaidizi wake kwa mashirika ya kiraia. REUTERS/Souleymane Ag Anara
Matangazo ya kibiashara

Kiwango cha wastani cha misaada ya maendeleo ya Denmark kwa Mali ni sawa na euro milioni 40 kila mwaka. Bajeti hii imetengwa kwa ajili ya kufadhili mashirika yasiyo ya kiserikali - ya Mali au kutoka nchini Denmark - lakini pia kwa Wizara ya Utawala ya Mali au hata kwa jamii.

Msaada huu kwa hiyo sasa umesitishwa na Copenhagen ambayo, kulingana na taarifa iliyotolewa na Waziri wa Maendeleo katika vyombo vya habari vya Denmark, inataka kuendeleza miradi yake ya kibinadamu na msaada wake kwa mashirika ya kiraia. Lakini ushirikiano na wizara kuu "unarejeshwa kwenye kabatini na ni mada ya kutafakari upya, na Umoja wa Mataifa na Umoja wa Ulaya. »

Uamuzi huu unakuja huku matangazo yakitarajiwa kutoka Ufaransa na nchi nyingine za Ulaya zinasaidia Mali na kikosi cha Takuba, mafunzo ya kijeshi ya EUTM, lakini pia na Minusma, ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo.

Sehemu ya misaada ya kimataifa katika bajeti ya serikali ya Mali inakadiriwa kuwa 30%. Msaada wa maendeleo wa Denmark kwa Burkina Faso pia umesitishwa, kutokana na mapinduzi ya kijeshi ya Januari 24.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.