Pata taarifa kuu

Je, Kinshasa inachukukliaje kupelekwa kwa wanajeshi wa Angola mashariki mwa DRC?

Bunge la Angola linatazamiwa kujadili Ijumaa hii ombi la kutumwa kwa kikosi cha kijeshi mashariki mwa DRC. Kutumwa huku kulitangazwa siku chache zilizopita na Rais wa Angola, João Lourenço, ambaye pia ni rais wa sasa wa Jumuiya ya kimataifa ya ukanda wa Maziwa Makuu na mpatanishi wa mgogoro wa DRC.

Wapiganaji wa M23 wakiwa barabarani nchini DRC, baada ya kuondoka Kibumba, Desemba 23, 2022.
Wapiganaji wa M23 wakiwa barabarani nchini DRC, baada ya kuondoka Kibumba, Desemba 23, 2022. AP - Moses Sawasawa
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu mjini Kinshasa, Patient Ligodi

Wabunge wa Angola kuidhinisha ombi hili ni lazima, lakini haitakiwi kuleta matatizo yoyote. Je, nchini DRC, mamlaka za Kongo zinaonaje misheni na mamlaka ya kikosi hiki?

Kwa upande wa Kinshasa wanasema kikosi cha Angola hakiji kupigana mashariki mwa DRC dhidi ya kundi la waasi la M23 wala dhidi ya makundi mengine yoyote. Kikosi hiki kinakuja kutekeleza utaratibu wa ukaguzi uliotolewa na mchakato wa Luanda.

Katika Wizara ya Mambo ya Nje ya DRC, wanasisitiza juu ya hali ya kiufundi ya kutumwa huku. Wanajeshi hawa wa Angola wanatumwa mashariki mwa DRC kuandaa zoezi la kuwakusanya waasi wa M23 baada ya kusitishwa kwa mapigano na uwezekano wa kuondolewa kwa waasi hawa katika maeneo ambayo wamedhibiti katika miezi ya hivi karibuni.

Pointi nyingine ya ujumbe huo ni kuthibitisha madai na shutuma za uchokozi ambazo zinahatarisha uhusiano kati ya Kinshasa na Kigali.

Hata hivyo, katika hatua hii, hakuna idadi ya wanajeshi hao imetajwa wala muda wa misheni hii kutangazwa.

Kutumwa kwa kikosi hiki pia kutatokana na mawasiliano ya kidiplomasia yaliyofanywa kuhusiana na zioezi la kuondoka kwa waasi wa M23 katika maeneo wanayoshikilia.

Upatanishi wa Angola tayari umekutana na viongozi wa ukanda huu ukiwataka kuharakisha mchakato huo katika mazingira ya mvutano mpya kuhusu mji wa Sake, takriban kilomita 30 kutoka Goma.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.