Pata taarifa kuu
UCHAGUZI-SIASA

Sierra Leone: Ripoti ya waangalizi kuhusu Uchaguzi wa Mkuu yaibua hisia tofauti

Sierra Leone bado inasubiri matokeo ya uchaguzi mkuu wake. Matokeo ya mwisho yanatarajiwa kutangazwa leo Jumanne. Ripoti ya waangalizi wa kimataifa ilikuwa ukisubiriwa kwa hamu kuhusu uchaguzi huo. Wametoa ripoti ya uchunguzi wao, wakikaribisha jinsi uchaguzi huo ulifanyika kwa 'amani kwa ujumla', lakini pia vurugu na ukosefu wa uwazi katika mchakato wa uchaguzi.

Katika kituo cha kupigia kura mjini Freetown, Juni 24, 2023.
Katika kituo cha kupigia kura mjini Freetown, Juni 24, 2023. REUTERS - COOPER INVEEN
Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu maalum huko Freetwon, Marine Jeannin

Umoja wa Afrika na Jumuiya ya Madola walikuwa wa kwanza kuzungumza kuhusu uchaguzi mkuu nchini Sierra Leone.

"Ujumbe unabainisha kuwa licha ya changamoto kadhaa za awali, uchaguzi kwa ujumla ulifanyika kwa vizuri bila makabiliano yoyote na katika hali ya amani kwa kiasi kikubwa. Wapiga kura waliweza kushiriki kwa uhuru katika mchakato huo. Ujumbe unakaribisha hisia za uzalendo zinlizoonyeshwa na maafisa wa uchaguzi, vikosi vya usalama, raia kwa ujumla, ambao kwa pamoja walitekeleza jukumu lao katika kuhakikisha uchaguzi mkuu wa 2023 unafanyika kwa amani."

EU yakosoa kasoro ziizojitikeza

Jumuiya ya Uchumi ya Nchi za Afrika Magharibi, ECOWAS, inasikitishwa tu kwamba vyama vya siasa vilitangaza matokeo ya uchaguzi kabla ya Tume Huru ya Uchaguzi kutangaza rasmi.

Waangalizi wa Umoja wa Ulaya pia wamekaribisha "kura ya amani kwa ujumla", lakini wamekosoa mengine yaliyosalia.

“Waangalizi wetu walishuhudia ghasia na machafuko katika vituo saba wakati wa zoezi la upigaji kura na katika vituo viwili vya kupigia kura wakati wa kufunga na kuhesabu kura. Kabla ya uchaguzi huo, tume ya uchaguzi ilichukua hatua chanya ili kupunguza kasoro na makosa mbalimbali yaliyojitokeza katika hatua tofauti za mchakato wa uchaguzi. Hata hivyo, juhudi hizi ziligubikwa na ukosefu wa uwazi,” anasema mbunge wa Umoja wa Ulaya, Evin Incir.

Hatimaye, wameshutumu ghasia za baada ya uchaguzi… Vikosi vya usalama vilifyatua risasi katika makao makuu ya upinzani Jumapili jioni huko Freetown na kusababisha kifo cha mtu mmoja. Matokeo ya mwisho yanapaswa kutangazwa ndani ya saa chache zijazo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.