Pata taarifa kuu

Makabiliano yaripotiwa nchini Sudan kati ya jeshi na RSF

Nairobi – Mashambulio  ya anga, mapigano ya barabarani na mizinga imesikika katika mji mkuu wa Sudan Khartoum na mji mkuu wa kusini wa El-Obeid.

Wito umekuwa ukitolewa kwa majenerali hao wawili kusitisha mapigano
Wito umekuwa ukitolewa kwa majenerali hao wawili kusitisha mapigano AFP - ASHRAF SHAZLY
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa mkaazi wa eneo la El-Obeid, kilomita 350 (maili 220) kutoka kusini magharibi mwa Khartoum, mashambulio ya risasi yamelenga kambi za kijeshi za wapiganaji wa RSF.

Mapigano kati ya RSF na jeshi la kawaida, likiongozwa na majenerali wanaohasimiana, yamesababisha vifo vya takriban watu 3,000 na wengine zaidi ya milioni 3.3 kuyahama makazi yao tangu Aprili 15.

Aidha jeshi la serikali limeripotiwa kutekeleza mashambulio ya ndege za kivita kwenye kambi hizo za RSF wakati nao wakilezwa kujibu kwa risasi.

Kusini mwa Khartoum, walioshuhudia wameripoti mashambulio matatu ya anga asubuhi mapema wakieleza kwamba milipuko hiyo ilikuwa yakutisha.

Jeshi, siku ya Jumatano lilishutumu RSF kwa kulenga eneo la makazi katika mji mkuu katika shambulio la ndege isiyo na rubani ambapo raia 14 waliuawa na 15 kujeruhiwa.

Mzozo huo umekuwa ukiendelea kati ya mkuu wa jeshi Abdel Fattah al-Burhan na makamu wake wa zamani, kamanda wa RSF Mohamed Hamdan Daglo.

Mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita, imeanzisha uchunguzi mpya kuhusu madai ya uhalifu wa kivita huko Darfur, mwendesha mashtaka mkuu Karim Khan alisema wiki iliyopita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.