Pata taarifa kuu

Libya: UN na shirika la Hilali Nyekundu washindwa kuelewana juu ya idadi ya vifo Derna

Nchini Libya, ripoti ya mafuriko huko Derna bado hayajulikani. Kulingana na OCHA, shirika la Umoja wa Mataifa ambalo lilinukuu shirika la Hilali Nyekundu, takriban watu 11,300 wamefariki na 10,100 hawajulikani waliko katika mji wa Derna pekee. Hata hivyo, Septemba 17 saa sita mchana, msemaji wa shirika la Hilali Nyekundu alikanusha takwimu iliyotolewa na shirika la Umoja wa Mataifa.

Uharibifu uliosababishwa na mafuriko kutokana na kimbunga Daniel katika mji wa Derna, Septemba 14, 2023.
Uharibifu uliosababishwa na mafuriko kutokana na kimbunga Daniel katika mji wa Derna, Septemba 14, 2023. REUTERS - ESAM OMRAN AL-FETORI
Matangazo ya kibiashara

Jumapili hii, Septemba 17, shirika la Hilali Nyekundu nchini Libya imekanusha idadi ya vifo 11,300 kufuatia mafuriko ya Derna iliyohusishwa na shirika hilo na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA). “Tunashangaa kuona jina letu likichanganywa na takwimu hizi. Wanaongeza hali ya mkanganyiko, wakati watu wengi wako katika huzuni kutokana na kukosekana kwa ndugu zao,” msemaji wa shirika la Hilali Nyekundu nchini Libya Taoufik Chokri ameliambia shirika la habari la AFP kutoka Benghazi.

Tsunami

Kimbunga Daniel ambacho kilipiga Derna, mji wenye wakaazi 100,000, wakati wa usiku wa Jumapili kuamkia Jumatatu iilisababisha kupasuka kwa mabwawa mawili ya mto na kusababisha mafuriko ya ukubwa wa tsunami kando ya bonde linalovuka jiji hili. Waziri wa Afya wa utawala wa mashariki mwa Libya, Othman Abdeljalil, aliripoti siku ya Jumamosi jioni idadi ya vifo ya 3,252. Katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyochapishwa hapo awali, Shirika la Afya Duniani (WHO) lilisema kwamba miili ya watu 3,958 imepatikana na kutambuliwa, na kwamba "zaidi ya watu 9,000" bado hawajapatikana.

"Hali ya kibinadamu inasalia kuwa mbaya huko Derna," imesema OCHA, ambayo inaongeza mji huo hauna maji ya kunywa na angalau watoto 55 wamepewa sumu baada ya kunywa maji machafu.

Kazi ya timu za uokoaji na timu za utafutaji pia inakwamishwa na machafuko ya kisiasa yanayoripotiwa nchini humo tangu kifo cha dikteta Muammar Gaddafi mwaka 2011, huku serikali mbili hasimu, moja mjini Tripoli (magharibi), ikitambuliwa na Umoja wa Mataifa, na nyingine Mashariki. Mamlaka zinaonyesha kuwa pia walikuwa wameanza mchakato mgumu wa kutambua na kuorodhesha miili hiyo, mamia kadhaa ambayo ilizikwa haraka katika siku za kwanza.

(Pamoja na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.