Pata taarifa kuu

Mafuriko nchini Libya: Human Rights Watch yataka uchunguzi huru ufanyike

Shirika lisilo la kiserikali la Human Rights Watch linatoa wito wa kufanyika uchunguzi huru nchini Libya kuchunguza kushindwa katika usimamizi wa mafuriko ambayo yalikumba mashariki mwa nchi hiyo Septemba mwaka jana.

Muonekano wa mji wa Derna, Libya, ulioharibiwa na mafuriko.
Muonekano wa mji wa Derna, Libya, ulioharibiwa na mafuriko. © Jamal Alkomaty / AP
Matangazo ya kibiashara

Kupita kwa kimbunga Daniel na kuporomoka kwa mabwawa mawili usiku wa Septemba 10 hadi 11 kulisababisha uharibifu mkubwa na kusababisha vifo vya karibu watu 13,000 huko Derna, mashariki mwa Libya. Maafa hayo pia yalisababisha kuhama kwa wakaazi 43,000 kufuatia uharibifu wa vitongoji vyote. Mwanasheria Mkuu wa Libya ametangaza kufunguliwa kwa uchunguzi.

Uwazi

Lakini kwa mujibu wa shirika lisilo la kiserikali la Human Rights Watch, uchunguzi wa uwazi ni muhimu, kwa sababu mamlaka ya Libya ilipaswa kuwahamisha watu wanaoishi katika eneo lililojaa mafuriko huko Derna wakati dalili za kwanza za hatari zilipoonekana. “Naamini tunahitaji kupata undani wake ili kuelewa ni jinsi gani kudndoka huku kwa mabwawa mawili lingeweza kutokea. Daima kuna hatari kwamba hii itajirudia mahali pengine nchini Libya kwa sababu ya kutofanya kazi huku kunatokana na ushindani wa serikali, anasema Eric Goldstein, msemaji wa Human Rights Watch kwa Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini. Kuna haja ya kuwepo kwa uchunguzi, si katika ngazi ya kitaifa, lakini katika ngazi ya kimataifa. "

"Kupoteza kwa binadamu"

Kama hakikisho la uwazi na uaminifu, Human Rights Watch inasema imependekeza uchunguzi huu ufanywe na Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Kibinadamu. "Ninaamini kwamba kwa kweli hakuna chombo nchini Libya chenye uwezo wa kufanya uchunguzi ambao utatoa majibu yanayohitajika," anmeongeza Éric Goldstein. Ilikuwa ni zaidi ya maafa kutokana na hali ya hewa, pia ilikuwa ni kupoteza kwa binadamu. Hii ilitokea katika nchi ambayo kuna utawala usio na utendaji. Kulikuwa na maonyo mengi kwamba mabwawa yanahitaji ukarabati, ambao haukufanyika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.