Pata taarifa kuu

Zaidi ya watu 43,000 wakimbia makazi yao kufuatia mafuriko mabaya mashariki mwa Libya

Zaidi ya watu 43,000 wamekimbia makazi yao baada ya mafuriko mabaya ambayo yaliharibu mashariki mwa Libya, hasa mji wa Derna, Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) limesema lro Alhamisi Septemba 21, 2023. 

Derna, Libya: Timu za waokoaji zinafanya kazi ya kutoa miili ya wahanga wa kimbunga Daniel kutoka chini ya vifusi, Septemba 19, 2023.
Derna, Libya: Timu za waokoaji zinafanya kazi ya kutoa miili ya wahanga wa kimbunga Daniel kutoka chini ya vifusi, Septemba 19, 2023. REUTERS - ESAM OMRAN AL-FETORI
Matangazo ya kibiashara

"Kulingana na makadirio ya hivi punde ya IOM, watu 43,059 wamekimbia makazi yao kutokana na mafuriko kaskazini mashariki mwa Libya," shirika hili la Umoja wa Mataifa limesema katika ripoti yake ya hivi punde kuhusu hali ya mashariki mwa Libya baada ya kimbunga Daniel kupiga usiku wa Septemba 10 kuamkia 11 , hali ambayo ilisababisha vifo vya zaidi ya watu 3,300, kulingana na mamlaka.

Shirika la kimataifa la misaada la Msalaba Mwekundu limesema hali ya kiutu katika eneo lililokumbwa na mafuriko mashariki mwa Libya ni ya kutisha kwa wakati huu, watu wengi wakiwa bado hawapati mahitaji muhimu.

Jumatano wiki hii msemaji wa shirika hilo katika eneo la Mashariki ya Karibu na Kati, Imene Trabelsi alisema waathirika wa mafuriko ya wiki iliyopita wanakosa makazi sahihi, maji safi, umeme na huduma za mawasiliano.

Afisa huyo aidha alizungumzia ugumu wa kuwasiliana na timu zao zilizopo nchini Libya kutokana na changamoto za mitandao ya mawasiliano ya simu na intaneti.

Aligusia pia umuhimu wa kufukua miili ya wahanga wa mafuriko hayo waliofukiwa na vifusi wakati uwezekano wa kuwapata wakiwa hai ukizidi kufifia. Inakadiriwa zaidi ya watu 100,000 bado wamefukiwa na vifusi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.