Pata taarifa kuu

Maandamano yanaendelea kusini mwa Libya: Mitambo miwili ya mafuta bado inafungwa

Maandamano ya kupinga kuwepo kwa matakwa ya kijamii yanaendelea kusini mwa Libya na kupelekea kufungwa kwa visima viwili vya mafuta vilivyoko katika eneo la Ubari. Libya inazalisha mapipa milioni 1.9 ya mafuta kwa siku, 300,000 kutoka Hifadhi ya mafuta ya al-Sharara, mojawapo ya mitambo mikubwa zaidi nchini humo, na mengine kutoka mtambo wa el-Feel. Maandamano haya pia yanaonyesha mgawanyiko wa kisiasa kati ya mamlaka mbili zinazofanana zinazowania mamlaka nchini.

Hifadhi ya mafuta ya al-Sharara nchini Libya, kilomita 900 kusini mwa Tripoli.
Hifadhi ya mafuta ya al-Sharara nchini Libya, kilomita 900 kusini mwa Tripoli. © REUTERS/Ismail Zitoun
Matangazo ya kibiashara

Kujenga hospitali huko Oubari, kuajiri vijana waliobobea katika sekta ya mafuta, kuweka kiwanda maalum cha kusafisha mafuta huko Fezzan ili kufidia upungufu wa kudumu wa gesi na petroli pamoja na ukarabati wa miundombinu, haya ni madai ya wakazi wanaozuia Hifadhi ya mafuta: "hii ndiyo kadi pekee tunayopaswa kuweka shinikizo kwa Tripoli ili kupata haki zetu," anasema Abou Bakr Abou Setta, kiongozi wa jamii ya watu kutoka  Fezzan.

Serikali ya Dbeibah imetoa wito wa "kutafakari" na kutohusisha uzalishaji wa mafuta katika aina hii ya tatizo.

Ikumbukwe kwamba hali hii inakuja katika kutoelewana kamili kati ya taasisi za Libya juu ya makubaliano yaliyotiwa saini kwa upande mmoja na Dbeibah, Waziri Mkuu ambaye mamlaka yake yamemalizika kwa zaidi ya mwaka mmoja, na muungano wa kimataifa. Lengo: kuendeleza utafiti wa hidrokaboni katika Hifadhi ya mafuta ya Hamada si mbali na Tripoli. Uamuzi uliopingwa na Bunge na Baraza Kuu la Nchi. Kwao, mkataba huo unatia shaka na unalenga kumsaidia Dbeibah kusalia madarakani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.