Pata taarifa kuu

Mfahamu Hage Gottfried Geingob, Mwanaharakati wa uhuru tangu alipokuwa na umri mdogo

Hage Gottfried Geingob ambaye alizaliwa kaskazini mwa Namibia mwaka 1941, alianzisha uanaharakati akiwa na umri mdogo, akitaka kukomeshwa kwa utawala wa kibaguzi wa Afrika Kusini ambao wakati huo ulitawala eneo la Namibia, kabla ya kwenda uhamishoni kwa karibu miongo mitatu.

Licha ya sintohafamu nchini mwake, Hage Gottfried Geingob alishinda muhula wa pili mnamo 2019, hata hivyo akipata kura chache kuliko hapo awali (56%).
Licha ya sintohafamu nchini mwake, Hage Gottfried Geingob alishinda muhula wa pili mnamo 2019, hata hivyo akipata kura chache kuliko hapo awali (56%). AFP PHOTO/JORDAANIA ANDIMA
Matangazo ya kibiashara

 

Nchini Marekani, aliendeleza kwa bidii uhuru wa Namibia na kuwakilisha vuguvugu la ukombozi wa ndani, SWAPO - chama tawala cha sasa, katika Umoja wa Mataifa na Amerika.

Mwaka 1989, alirejea Namibia, mwaka mmoja kabla ya uhuru wa nchi yake na kuteuliwa kwa mara ya kwanza kama Waziri Mkuu.

Alihikilia nafasi hiyo kwa miaka kumi na mbili, rekodi ya kuishi maisha marefu nchini Namibia, kabla ya kushikilia tena wadhifa huo mwaka wa 2012.

Kisha alichaguliwa kuwa rais mwaka wa 2014 kwa 87% ya kura, alijikuta muhula wake wa kwanza ukigubikwa na mdororo wa uchumi, kiwango kikubwa cha ukosefu wa ajira na shutuma za vitendo vya kukosa uaminifu.

Mnamo mwaka wa 2019, nyaraka zilizotangazwa kwa umma na WikiLeaks zilipendekeza kwamba maafisa wa serikali walipokea hongo kutoka kwa kampuni ya Iceland ambayo ilitaka kupata ufikiaji wa rasilimali za uvuvi za Namibia.

Licha ya sintohafamu, Hage Gottfried Geingob alishinda muhula wa pili mnamo 2019, hata hivyo akipata kura chache kuliko hapo awali (56%).

(Pamoja na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.