Pata taarifa kuu

Sudan: Ishirini na nane wauawa katika shambulio la RSF katika kijiji cha Um Adam

Takriban watu 28 waliuawa nchini Sudan wakati wa shambulio lililofanywa na vikosi vya wanamgambo kwenye kijiji kimoja kusini mwa mji mkuu Khartoum, mashirika mawili yanayounga mkono demokrasia ya Sudan liliripoti siku ya Jumapili.

Zaidi ya 70% ya vituo vya afya vya Sudan havina huduma, kulingana na Umoja wa Mataifa, wakati vile vinavyofanya kazi vinapokea mara kadhaa idadi kubwa ya watu waliojeruhiwahuku vikiwa na rasilimali chache sana. Pande zote mbili zimeshutumiwa kwa uhalifu wa kivita, ikiwa ni pamoja na kuwalenga raia, ulipuaji wa mabomu kiholela katika maeneo ya makazi, na uporaji na kuzuia misaada ya kibinadamu.
Zaidi ya 70% ya vituo vya afya vya Sudan havina huduma, kulingana na Umoja wa Mataifa, wakati vile vinavyofanya kazi vinapokea mara kadhaa idadi kubwa ya watu waliojeruhiwahuku vikiwa na rasilimali chache sana. Pande zote mbili zimeshutumiwa kwa uhalifu wa kivita, ikiwa ni pamoja na kuwalenga raia, ulipuaji wa mabomu kiholela katika maeneo ya makazi, na uporaji na kuzuia misaada ya kibinadamu. © Florence Miettaux / RFI
Matangazo ya kibiashara

Kikosi cha Rapid Support Forces (FSR), kinachokabiliana na jeshi la serikali kwa mwaka mmoja, "kilishambulia kijiji cha Um Adam" kilomita 150 kusini mwa Khartoum, shirika ambalo linasimamia misaada ya pande zote kati ya wakaazi lilisema mapema Jumapili. Shambulio hilo lilitekelezwa siku ya Jumamosi na kusababisha vifo vya takriban watu 28, "wanakijiji wasio na hatia", pamoja na watu 240 kujeruhiwa, Kamati ya Madaktari wa Sudan, shirika jingine huru na linalounga mkono demokrasia, lilisema Jumapili jioni.

"Kuna idadi ya watu waliofariki na kujeruhiwa kijijini hapo ambao hatujaweza kuwahesabu kutokana na kushindwa kufika katika vituo vya afya na kufuatilia matatizo wakati wa shambulio hilo," liliongeza shirika hili, likilaani "mauaji yaliyofanywa na Kikosi cha Msaada wa Haraka." ”. Kamati ya Upinzani ya eneo hilo, kwa upande wake, iliripoti Jumapili asubuhi "zaidi ya watu 200 waliojeruhiwa, wengine vibaya na wengine ambao walipata majeraha madogo, na zaidi ya watu 20 kuuawa", kabla ya kurekebisha idadi ya vifo hadi 25 katikati ya mchana.

Chanzo cha hospitali katika hospitali ya Manaqil, umbali wa kilomita 80, kililiambia shirika la habari la AFP siku ya Jumapili asubuhi kwamba "wamepokea watu 200 waliojeruhiwa, wengine walifika wakiwa wamechelewa". "Tunakabiliwa na uhaba wa damu na hatuna wafanyakazi wa afya kutosha," kilionya.

70% ya miundo ya afya haitumiki

Vita nchini Sudan vilianza Aprili 15, 2023 kati ya jeshi, chini ya uongozi wa Jenerali Abdel Fattah al-Burhane, na wanamgambo wa FSR, wakiongozwa na naibu wake wa zamani Jenerali Mohamed Hamdane Daglo. Vita hivi vimesababisha vifo vya maelfu ya watu na zaidi ya watu milioni 8.5 kuyahama makaazi yao, kulingana na Umoja wa Mataifa. Pia kwa kiasi kikubwa iliharibu miundombinu ya nchi, na kuipeleka kwenye ukingo wa njaa.

Zaidi ya 70% ya vituo vya afya vya Sudan havina huduma, kulingana na Umoja wa Mataifa, wakati vile vinavyofanya kazi vinapokea mara kadhaa idadi kubwa ya watu waliojeruhiwahuku vikiwa na rasilimali chache sana. Pande zote mbili zimeshutumiwa kwa uhalifu wa kivita, ikiwa ni pamoja na kuwalenga raia, ulipuaji wa mabomu kiholela katika maeneo ya makazi, na uporaji na kuzuia misaada ya kibinadamu.

Tangu kuchukua udhibiti wa jimbo la Al-Jazeera karibu na Khartoum mwezi Desemba, RSF imezingira na kushambulia vijiji vizima kama Um Adam. Kufikia mwezi wa Machi, angalau vijiji na maeneo 108 kote nchini yamechomwa moto na "kuharibiwa kwa kiasi au kabisa", kulingana na Kituo cha Ustahimilivu wa Taarifa, mtandao wa wachunguzi huru walioko nchini Uingereza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.