Pata taarifa kuu

Vita nchini Sudani: Mashirika ya kiraia yakutana sambamba na mkutano wa kimataifa

Mkutano sambamba ulifanyika tarehe 15 Aprili mjini Paris kando ya mkutano wa kimataifa wa kibinadamu kwa Sudan katika Taasisi ya Ulimwengu wa Kiarabu. Mkutano huo ulileta pamoja takriban wadau arobaini tofauti kutoka mashirika ya kiraia.

Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Sudan Abdalla Hamdok, mnamo mwaka 2021.
Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Sudan Abdalla Hamdok, mnamo mwaka 2021. AP - Christophe Ena
Matangazo ya kibiashara

Miongoni mwa wadau hawa wanawake na wanasiasa, viongozi wa kimila au kidini, wanaharakati wa vyama vya wafanyakazi na waandishi wa habari walikuwa hasa Waziri Mkuu wa zamani Abdallah Hamdok, Maryam Sadek al Mahdi anayewakilisha chama cha Umma na sultani wa jumuiya ya Masalit.

Vuguvugu la Haki na Usawa liliwakilishwa na katibu mkuu wake, Ahmed Mohamed Tugod Lissan. Anatoa tathmini chanya ya kwanza ya mkutano huu. "Mkutano ulikuwa mzuri. Lengo lake kuu lilikuwa kuleta pamoja idadi kubwa ya vyama vya kisiasa kutafakari njia za kuendeleza mchakato wa kisiasa nchini Sudan. Wakati huo huo, suala hili lilijadiliwa ndani ya mfumo wa usitishaji mapigano, na haswa kushughulikia maswala ya kibinadamu. "

Katibu mkuu wa vuguvugu la Haki na Usawa anaeleza kuwa majadiliano hayo yalilenga masuala matatu muhimu: “La kwanza: kufikiria jinsi ya kukomesha uhasama na kanuni za kimsingi ambazo zingesaidia pande zinazokinzana kuingia katika mchakato unaopelekea usitishaji vita na kukomesha uhasama. La pili linajumuisha kufikiria jinsi ya kukubaliana juu ya mradi wa kisiasa ambao huanzisha kipindi cha baada ya vita. La mwisho: kufikiria jinsi ya kujenga tena nchi baada ya kumalizika kwa vita. "

"Mkutano huu wa misaada ya kibinadamu unakuja wakati mwafaka"

Waziri Mkuu wa zamani Abdallah Hamdok sasa anaongoza Taqaddum, uratibu wa vikosi vya kiraia vya kidemokrasia. Kama wahusika wote katika mashirika ya kiraia nchini Sudan, amesisitiza juu ya haja ya utatuzi wa amani wa mzozo huo. Anaishukuru jumuiya ya kimataifa kwa kuandaa mkutano wa kibinadamu huko Paris: "Mkutano huu unakuja wakati ambapo Sudan inahitaji sana msaada wa kimataifa, kwa sababu tunapitia hali mbaya. Inavuta hisia za ulimwengu kwa maafa yanayoikabili Sudan na ambayo yanatishia maisha ya mamilioni ya watu. Zaidi ya Wasudan milioni 20 wako katika hatari ya kufa njaa. Mkutano huu wa misaada ya kibinadamu unakuja wakati mwafaka. Tunashukuru Ufaransa, Ujerumani na Umoja wa Ulaya kwa kuandaa mkutano huu. "

Waziri Mkuu huyo wa zamani anaeleza kuwa anataka kuwafikia Wasudan wengi iwezekanavyo na muungano wake ili kuelekea kwenye amani: “Hatujawahi kudai kuwawakilisha Wasudan wote, lakini tunanyoosha mkono wetu kwa wale wote wanaofanya kazi ya kumaliza vita na kurejesha mabadiliko ya kiraia na kidemokrasia. Tunakaribisha mipango yote ya amani inayotaka kukomesha vita na tunafanya kazi pamoja kuhamasisha eneo kubwa zaidi katika juhudi za kumaliza vita. Katika mkutano wetu wa mwisho mjini Addis Ababa, tuliwasilisha dira ya kisiasa ambayo inajumuisha mwito wa mkutano unaoleta pamoja vyama vyote vya Sudan. Tunajitahidi kufikia mafanikio ya mpango huu na tutafikia pande zote. "

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.