Pata taarifa kuu
MAREKANI-Mauaji-Usalama

Marekani : Texas yakumbwa na mauaji

Mtu mmoja amewaua watoto wanne na watu wazima wawili wakati walipokua katika mabishano ya kifamilia jumatano wiki hii katika jimbo la Texas kusini mwa Marekani, kabla ya kukamatwa na polisi na kuwekwa jela, chanzo cha polisi kimeeleza.

Rais wa Marekani, Barack Obama.
Rais wa Marekani, Barack Obama. REUTERS/Larry Downing
Matangazo ya kibiashara

Mwanamke mmoja amejeruhiwa na risase na wakati huu yuko katika hali ya mahututi, mkuu wa polisi, Ron Hickman, ameeleza. Ron Hickman amesema watu wazima hao waliouawa ni wanaume.

Kabla ya kupelekwa hospitalini, mwanamke huyo aliyejeruhiwa amesema mhalifu alietekeleza mauaji hayo ni kutoka familia moja na watu waliouawa.

Askari polisi walimfutilia mtu huyo kwa muda wa dakika ishirini, baada ya kutekeleza uhalifu huo, na baadae alizingirwa na askari polisi 50, huku akinyoshewa bunduki kishwani.

Mhalifu amekamatwa na amewekwa jela, ofisi ya Sherif ya shirika la kihisani Harris imesema kupitia mtandao wa Twitter.

Vitendo vya mauaji vimekua sugu nchini Marekani.
Vitendo vya mauaji vimekua sugu nchini Marekani. REUTERS/WNBC/Handout

Vitendo hivyo vya mauwaji kwa kutumia silaha za moto vimekua sugu nchini Marekani.

Mwanzoni mwa mwezi juni, rais wa Marekani Barack Obama aliwatolea wito raia wake kufanya “uchunguzi wa akili” kuhusu silaha za moto.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.