Pata taarifa kuu
ISRAEL-PALESTINA

Vurugu zaidi zaenea Gaza, wapalestina 157 wauawa

Licha ya dunia kuiomba Israel na Hamas kukomesha uhasama jana Jumamosi, vurugu zimeenea huku idadi ya waliouawa kwa mashambulizi ya Israel ikiongezeka na kufikia 157 na wanamgambo wa Gaza wakiendelea kurusha roketi zaidi.

Athari ya mashambulizi ya anga yaliyofanywa na  Israel siku ya Jumamosi
Athari ya mashambulizi ya anga yaliyofanywa na Israel siku ya Jumamosi AFP PHOTO / JACK GUEZ
Matangazo ya kibiashara

Pande zote mbili zimetupilia mbali mwito wa jamii ya kimataifa wa kusitisha mapigano na Israel imeendelea kuongeza vikosi vya askari na silaha kwenye mpaka wa Gaza kwa ajili ya maandalizi ya shambulizi la ardhini nakuwaonya wapalestina Kaskazini mwa Gaza kuondoka katika makaazi yao.

Pamoja na wapalestina 157 kuuawa na kukiwa hakuna m Israel aliyeuawa,Baraza la Usalama bila kupingwa limetoa wito kwa Israel na Hamas kuheshimu "sheria za kimataifa" na kukomesha mauaji.

Mashambulizi ya jana Jumamosi, ambayo kitengo cha huduma za dharura cha Gaza kimesema yamepiga msikiti na kituo cha walemavu miongoni mwa maeneo lengwa mengine, yalisababisha jumla ya vifo tangu kuanza kwa Operesheni kinga kingo za Israeli siku ya Jumanne kufikia watu 127 jana Jumamosi.

Rais wa Marekani Barack Obama alimpigia simu Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu siku ya Ijumaa na Washington ikajitolea kutumia ushawishi wake kurejesha utulivu Mashariki ya Kati .

Lakini akizungumza katika mkutano wa wanahabari mjini Tel Aviv siku ya Ijumaa, Netanyahu alisema Israel haitakomesha kampeni ya kijeshi mpaka ifikie mafanikio ya lengo lake la kuzuia mashambulizi ya kigaidi yanayofanywa na kundi la Hamas.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.