Pata taarifa kuu
BRAZIL-Uchaguzi-Siasa

Brazil: wanawake washindana kwa kugombea kwenye uchaguzi wa urais

Pambano kati ya rais anayemaliza muda wake Dilma Rousseff na Marina Silva, ambaye anapewa nafasi kubwa ya kushinda uchaguzi wa Oktoba 5 linaendelea kushika kasi wakati uchaguzi ukikaribia.

Dilma Roussef (kushoto) pamoja na  Marina silva (kulia), wakati wa mjadala uliyorushwa kwenye televisheni Oktoba 2 mwaka 2014, kabla ya duru ya kwanza ya uchaguzi wa urais
Dilma Roussef (kushoto) pamoja na Marina silva (kulia), wakati wa mjadala uliyorushwa kwenye televisheni Oktoba 2 mwaka 2014, kabla ya duru ya kwanza ya uchaguzi wa urais REUTERS/Ricardo Moraes
Matangazo ya kibiashara

Dilma Rousseff, ambaye anagomea muhula wa pili, anaendelea kupoteza kulingana na matokeo ya hivi karibuni.

Wagombea wote wawili walikua wafuasi wa rais wa zamani wa Brazil, Lula, kwenye chama cha Leba (PT). Mmoja kati yao bado ni mfuasi wa chama hicho , mwengine alijiondoa tangu kitambo. Haijajulikana iwapo kifo cha Eduardo Campos, aliye kuwa mgombea kwa tiketi ya chama cha Kisoshalisti (PSB), ndio kilipelekea Marina Silva anachukua mstari wa mbele kwa kugomea urais.

Eduardo Campos alifariki kufuatia ajali ya ndege mwezi Agosti mwaka 2014. Hata hivo rais anayemaliza muda wake, Dilma Rousseff bado ana matumaini ya kuendelea kuliongoza taifa la Brazil kwa kipindi cha miaka minne ijayo.

Iwapo Marina Silva atashinda uchaguzi, atakua rais wa kwanza mweusi kuliongoza taifa la Brazil. Marina Silva, mwenye umri wa miaka 56, amesema ana imani kuwa atakamilisha ndoto yake ya kuwa rais wa Brazil. Mgombea huyo alizaliwa katika familia masikini ya watu weusi, huku akiwa mama wa watoto 11. Marina Silva anashirikiana na familia yake kwa kuendesha shughuli za kilimo. Marina Silva ana miaka 16 baada ya kujua kusoma na kuandika.

Marina Silva ni Seneta, alichaguliwa kwenye nafasi hiyo akiwa na umri wa miaka 36, kabla ya kuwa Waziri wa mazingira mwaka 2003 hadi 2008 katika serikali ya rais Lula Da Silva.

Mwaka 2008, Marina Silva alitofautiana na Dilma Rousseff, ambaye alikua mkurugenzi kwenye Ofisi ya rais wa Brazil, Lula, baada ya kuteuliwa kuwa Waziri wa nishati. Tofauti hizo zilipelekea Marina Silva anachukua uamzi wa kujiuzulu kwenye wadhifa wake, na baadaye alijiunga na vyama vinne vya siasa kwa muda wa miaka 3. Uchaguzi wa Urais nchini Brazili unatazamiwa kufanyika kesho Jumapili Oktoba 5.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.