Pata taarifa kuu
CANADA-Usalama

Canada: milio ya risase yasikika ndani ya jengo la Bunge

Hali ya wasiwasi imetokea Jumatano mchana Oktoba 22 katika mji wa Ottawa, nchini Canada, baada ya miliyo mingi ya risase kusikika pembezuni mwa eneo la kibiashara katikati ya mji na ndani jengo la Bunge. Afisa wa Bunge amejeruhiwa pia kwa risase.

Kikosi maalumu cha polisi kimezingira jengo la Bunge la mji wa Ottawa baada ya miliyo ya risase kusikika ndani ya jengo hilo.
Kikosi maalumu cha polisi kimezingira jengo la Bunge la mji wa Ottawa baada ya miliyo ya risase kusikika ndani ya jengo hilo. REUTERS/Chris Wattie
Matangazo ya kibiashara

Mwanajeshi mmoja wa Canada aliye jeruhiwa kwa risase akiwa mbele ya mnara wa ukumbusho wa vita vya dunia, amefariki.

Mmoja wa watu waliyofyatua risase hizo ameuawa kwa kupigwa risase na vyombo vya usalama. Polisi inawasaka watu wengine waliyohusika na kitendo hicho.

Waziri wa kazi, Jason Kenney , amebaini kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter kwamba mwanajeshi aliye fariki kutokana na majeraha ya risase alikua mlinzi kwenye eneo hilo la ukumbusho.

Mpaka sasa hali ya wasiwasi imeendelea kutanda katika mji mkuu wa canada. Kikosi maalumu cha polisi kimezingira jengo la Bunge, huku kikitenga eneo la usalama katika kata zote za mji wa Ottawa.

Watu wengi wameondolewa ndani ya jengo la Bunge, hususan Waziri mkuu, Stephen Harper, viongozi wa upinzani, Thomas Mulcair na Justin Trudeau wamewekwa katika eneo salama. Hata hivyo baadhi ya wabunge bado wamo ndani ya jengo la Bunge. Polisi imewataka wasaliye ndani ya jengo hilo na wakae mbali na madirisha.

Polisi imewataka pia wakaazi wa mji wa Ottawa kukaa mbali na madirisha, ikibaini kwamba mmoja wa watu wenye silaha amekimbilia juu ya paa ya jengo la Bunge.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.