Polisi nchini Canada wamkamata mtuhumiwa aliyeua askari watatu
Polisi nchini Canada imetangaza kuwa inamshikilia raia mmoja anayetuhumiwa kuhusika na mauaji ya polisi watatu na kujeruhi wengine kadhaa kwenye eneo la Moncton mjini New Brunswick.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Polisi kwenye mji wa New Brunswick kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter leo asubuhi wameandika kuwa Justin Bourque alikamatwa usiku wa kuamkia leo kwenye eneo la Moncton.
Taarifa ya kukamatwa kwa mtuhumiwa huyu imetolewa baada ya kufanyika kwa operesheni kubwa na ya kina na polisi wa Canada kuendesha msako wa kumkamata Bourque.
Shule na ofisi za Serikali zilikuwa zimefungwa kwenye mji huo na wananchi walitakiwa kutotembea hovyo usiku na kujifungia majumbani mwao kwakuwa mtuhumiwa huyu alikuwa amejihami kwa silaha nzito.
Kwenye taarifa yao, Polisi kwenye mji wa Moncton wameataka wananchi hivi sasa kutoka kwenye nyumba zao kwakuwa tishio la usalama limemalizwa.
Baadhi ya mashuhuda wa tukio hili wamesema kuwa walishuhudia Polisi wakimkamata mtuhumiwa huyu na kumchukua kwa gari.