Pata taarifa kuu
CANADA

Polisi nchini Canada wafanikiwa kulikamata genge la watengeneza filamu za ngono na kuwatumia watoto

Polisi nchini Canada wamefanikiwa kuwakamata watu zaidi 341 wanaodaiwa kushiriki kwenye uandaaji wa filamu za ngono zinazowahusisha watoto wadogo, hatua inayokuja wakati huu nchi hiyo ikiendesha operesheni maalumu kuwasaka wamiliki wa mitandao ya ngono zinazohusisha watoto wadogo. 

Mkuu wa Polisi nchini Canada akizungumza na polisi kueleza namna watu hao walivyokamatwa
Mkuu wa Polisi nchini Canada akizungumza na polisi kueleza namna watu hao walivyokamatwa Reuters
Matangazo ya kibiashara

Polisi nchini humo inasema kuwa miongoni mwa waliokamtwa kwenye operesheni hiyo, wamo pia askari polisi, madaktari, manesi, waalimu na hata wachungaji wa makanisa mbalimbali ambao wamekuwa wakishiriki katika uandaaji wa filamu hizo.

Inspecta wa polisi mjini Toronto, Beaven Desjardins amethibitisha kukamatwa kwa watu hao na kwamba wamefanikiwa kuwaokoa wasichana zaidi ya 386 ambao ni wasichana wadogo waliokuwa wakitumiwa kwenye kutengeneza filamu za ngono ambazo zinauzwa ulimwenguni hivi sasa.

Polisi wameongeza kuwa walifanikiwa kubaini mtandao wa watu wanaowahusisha watoto wadogo kwenye utengenezaji wa filamu hizo baada ya kutuma maofisa wake wa upelelezi ambao walifanikiwa kubaini mmiliki wa mtandao mmoja wa ngono ambaye walifanya nae mawasiliano kabla ya kutega mtengo uliowanasa watu wengine.

Hivi karibuni Serikali ya Canada ilitangaza kuanzisha operesheni maalumu dhidi ya watu wanaodaiwa kutengeneza filamu za ngono wakiwatumia wasichana wadogo kwenye filamu hizo jambo ambalo liliamsha hasira toka kwa wanaharakati waliotaka Serikali ichukue hatua.

Kwenye ripoti yao polisi wanasema kuwa walibaini kuwepo kwa mtandao wa www.azovfilms.com ambao hutumiwa na wamiliki wake duniani kote na watu wamekuwa wakituma maombi ya kununua filamu hizo ambazo wamekuwa wakitengeneza wakihusisha wasichana wadogo.

Tayari watu hao wamefunguliwa mashtaka mbalimbali ikiwemo kuendesha mtandao wa ngono, kuwahusisha wasichana wadogo kwenye utengenezaji wa filamu za ngono na pia kutoa rushwa kwa baadhi ya wazazi kuwaruhusu watoto wao kutengeneza filamu hizo pamoja na kujipatai fedha kinyume cha sheria.

Mashirika ya kutetea haki za binadamu duniani yamekuwa yakishinikiza Serikali ya Canada na mataifa mengine kufanya operesheni maalumu kuwasaka watu wanaotengeneza filamu za ngono na kuwahusisha wasichana wadogo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.