Pata taarifa kuu
Syria-Usalama

Marekani: hatuna vielelezo kuthibitisha athari za shambulizi la Raqa

Marekani imeeleza kuwa haina uthibitisho wa kuunga mkono madai ya kundi la Islamic State kwamba shambulizi la anga lililofanywa na muungano wa majeshi yanayoongozwa na marekani liliua mwanamke raia wa marekani ambaye alikuwa mateka wa kundi hilo nchini Syria.

Wanamgambo wa Islamic State nchini Syria
Wanamgambo wa Islamic State nchini Syria REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Wanajihadi hao wametaja jina la mwanamke huyo raia wa marekani kuwa ni Kayla Jean Mueller, na kuongeza kuwa amezikwa katik akifusi baada ya shambulizi kufanywa na ndege za kivita za katika jiji la Raqa nchini syria ambako kundi hilo wanauita mji mkuu.

Hata hivyo serikali ya Washington ilikataa kuthibitisha kifo hicho wakati jordan ambayo bado inauchungu wa kuuawa kwa rubani wake ikikataa madai hayo kwa kuyaita ni mbinu ya kizamani na dhaifu.

Wanajihadi hao kupitia mtandao wao walieleza kuwa hakuna mpiganaji aliyeuawa isipokuwa mwanamke ambaye alikuwa raia wa Marekani na mateka wao huko Syria.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.