Marekani: maandamano mapya yatokea Baltimore
Maandamano mapya yametokea katika mji wa Baltimore nchini Marekani kufuatia kifo cha Freddie Gray, kijana mweusi aliyefariki kutokana na majeraha akiwa mikononi mwa polisi.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Raia wengi wameingia mitaani, wakionyesha ujasiri wao licha ya hali mbaya ya hewa iliyoripotiwa katika mji huo.
Awali maelfu ya watu waliandamana katika miji mikubwa nchini Marekani kushinikiza polisi kuacha kuwanyanyasa watu wenye asili ya Afrika.
Maandamano hayo yalifanyika baada ya kijna mmoja mwenye asili ya Kiafrika kuuawa alipokuwa anazuiliwa na polisi katika mji wa Baltimore katika jimbo la Maryland juma lililopita.
Katika mji wa Baltimore waandamanaji waliokuwa na hasira walihakikisha kuwa shughuli zote zinasimama wakati wa maandamano hayo.
Miji ambayo imeshuhudia maandamano hayo mbali na Baltimore ni pamoja na New York, Boston na jiji kuu la Washington DC.
Maandamano ya Alhamisi wiki hii yaliekuwa ya amani katika miji yote.
Siku tatu zilizopita katika mji wa Baltimore polisi walikabiliana na waandamanaji ambao waliamua kupora na kuvamia watu baada ya kuawa kwa kijana huyo mweusi.
Matokeo ya mwanzo ya uchunguzi wa polisi wa jinsi kijana wa miaka ishirini na mitano mwenye asili ya weusi alivyouawa bado hayajawekwa hadharani.