Pata taarifa kuu
CUBA-MAREKANI-PAPA-USHIRIKANO

Cuba: Papa atamatisha ziara yake kabla ya kusafiri kwenda Marekani

Idadi kubwa ya raia wa Marekani wamezuzungukwa na matumaini, lakini pia watu wachache wamejizuia kutoa msimamo wao, ambapo Papa Francis, kutoka Cuba, atakua Washington, nchini Marekani Jumanne wiki hii.

Papa Francis azungukwa na watoto, Septemba 21, 2015 katika mahala patakatifu pa Bikira "del Cobre" katika mji wa Santiago nchini Cuba.
Papa Francis azungukwa na watoto, Septemba 21, 2015 katika mahala patakatifu pa Bikira "del Cobre" katika mji wa Santiago nchini Cuba. Jean-Louis DE LA VAISSIERE | AFP
Matangazo ya kibiashara

Ni kwa mara ya kwanza kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki kufanya ziara nchini Marekani.

Papa Francis atapokelewa na Rais wa Marekani Barack Obama na mkewe.

Papa atatamatisha ziara yake ya masaa 72 Jumanne wiki hii nchini Cuba (kisiwa cha kikomunisti), nchi ambayo ilifufua hivi karibuni uhusiano wake Marekani kwa mchango mkubwa wa msuluhishi kutoka Vatican na Papa kutoka Argentina.

Ni katika mji wa Santiago nchini Cuba, ambapo kunapatikana bandari kubwa ya kisiwa hicho, kulikoanzishwa harakati za ukombozi wa Cuba, karibu na kambi ya majeshi ya Marekani ya Guantanamo, Papa Francis alipokelewa na kusherehekewa kwa muda wa siku nne.

Papa mwenye umri wa miaka 78 sasa, atasherehekea Misa ya mwisho ya ziara yake katika mahali patakatifu pa Bikira "del Cobre", katika milima ya kijani karibu na mji, na ambapo siku moja kabla aliongoza maombi kwa mustakabali wa watu wa Cuba.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.