Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN-NATO-MAREKANI-TALIBAN-USALAMA

Afghanistan: Taliban wadai kudungua ndege ya Marekani C-130

Kundi la Taliban limesema leo Ijumaa kuwa limeidungua ndege aina ya C-130 iliyo kuwa ikisafirisha wanajeshi wa Marekani mashariki mwa Afghanistan usiku wa kuamkia leo Ijumaa. Ajali hiyo imewaua, kwa mujibu wa jeshi la Marekani, watu 11.

Ndege ya Marekani ya kusaririsha wanajeshi C-130 ikitua uwanja wa ndege wa Kabul, Agosti 19, 2012.
Ndege ya Marekani ya kusaririsha wanajeshi C-130 ikitua uwanja wa ndege wa Kabul, Agosti 19, 2012. AFP/AFP/Archives
Matangazo ya kibiashara

" Wapiganaji wetu ameidungua ndege ya kijeshi ya Mareknani katika eneo la Jalalabad", Msemaji wa Taliban, Zabihullah Mujahid. amesema kwenye twitter. Ujumbe wa NATO hadi sasa haujato maelezo ya sababu za ajali hiyo.

Ajali ya C-130 usiku wa Alhamisi kuamkia Ijumaa imesababisha vifo vya watu 11, ikiwa ni pamoja na askari sita wa Marekani, hapo awali afisa mmoja kwenye wizara ya ulinzi wa Marekani alitangaza.

" Wafanyakazi na watu wote waliokuweno katika ndege hiyo wamefariki ", amesema afisa wa jeshi la nchi kavu la Marekani Brian Tribus, ambaye amesema kuwa askari sita wa Marekani na makandarasi watano ambao walikua raia wamefariki katika ajali hiyo.

Ajali ilitokea katika uwanja wa ndege wa Jalalabad majira ya usiku wa manane saa za Afghanistan (sawa na saa 1:30 saa za kimataifa Alhamisi wiki hii).

Sababu za ajali hazijajulikana. Katika uwanja huo wa ndege kuna kambi ya jeshi ambayo imekua ikishambuliwa mara kadhaa.

Wanajeshi hao walikua wakishiriki katika ujumbe wa Umoja wa nchi za kujihami za magharibi (NATO) unaojulikana kama "Msaada uliyopatiwa suluhu", wenye leno la kutoa ushauri na mafunzo kwa majeshi ya Afghanistan ambayo kwa sasa yanakabiliana peke yake katika mstari wa mbele dhidi ya wapiganaji wa kundi la Taliban waasi tangu kumalizika kwa ujumbe wa NATO wa kupambana, Desemba mwaka uliyopita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.