Pata taarifa kuu
INDIA

Anna Hazare ajiapiza kuongoza Mapinduzi nchini India

Mwanaharakati nguli nchini India Anna Hazare ameweka nadhiri ya kufanikisha mapinduzi nchini mwake wakati huu ambapo ameanza kutekeleza ahadi yake ya kufunga kula na kunywa kwa kipidi cha siku kumi na tano.

REUTERS/Adnan Abidi
Matangazo ya kibiashara

Hazare ambaye ameachiwa leo baada ya kukamatwa siku ya jumanne asubuhi kwa kosa la kuhitisha maandamano ya wafuasi wake bila ya kibali amesema huu ni wakati wa kuleta mabadiliko kwa taifa hilo.

Mwanaharakati huyo amepokelewa na maelfu ya wafuasi wake ambao walijitokeza katika Jiji la New Delhi kumlaki baada ya kuachiwa kwa makubaliano ya kupunguza ahadi yake ya kufunga kula na kunywa na kusalia siku kumi na tano.

Hazare amewaambia wafuasi wake waliojitokeza kuwa dunia inawaangalia kama sehemu ya mfano wa kuleta mapinduzi katika nchi hiyo bila ya kufanya machafuko kama ambavyo imezoeleka kwenye mataifa mengine.

Uamuzi wa Mwanaharakati Hazare umekuja kwa lengo la kuishinikiza serikali nchini India kutunga sheria kali zaidi dhidi ya viongozi ambao wanajihusisha na vitendo vya ulaji rushwa vilivyotawala kwenye taifa hilo.

Hazare aliitaka serikali kushughulikia mapendekezo yake ya namna ya kushughulikia suala la rushwa siku moja baada ya kufanyike kwa sherehe za kumbukumbu ya uhuru wa nchi hiyo ambapo Waziri Mkuu Manmohan Singh alitangaza mikakati ya kukabiliana na hali hiyo.

Serikali ya Waziri Mkuu Singh imekuwa ikikosolewa vikali kutokana na kushindwa kudhibiti vitendo vya ulaji rushwa ambavyo vimekuwa vikifanywa na baadhi ya mawaziri na hata kupoteza nafasi zao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.