Pata taarifa kuu
IRAQ-MAREKANI-ISIL-Usalama

Iraq: mvutano waibuka kati ya rais na waziri mkuu

Wakati hali ikiendelea kuwa mbaya kwenye uwanja wa mapambano nchini Iraq kufuatia kundi la Isil kuendelea kujizatiti katika miji kadhaa kaskazini mwa nchi hiyo, mvutano wa wazi umeibuka kati ya rais Fouad Masoum na waziri mkuu Nouri al Malik ambaye ametangaza jana kuwa atamfungulia mashtaka rais.

Wapiganaji wa kikurdi wakiangalia mji wa Makhmur katika jimbo la Erbil, kaskazini mwa Iraq, baada ya mashambulizi ya anga ya jeshi la Marekani.
Wapiganaji wa kikurdi wakiangalia mji wa Makhmur katika jimbo la Erbil, kaskazini mwa Iraq, baada ya mashambulizi ya anga ya jeshi la Marekani. REUTERS/Azad Lashkari
Matangazo ya kibiashara

Muda mfupi baada ya waziri mkuu wa Iraq Nouri al Malik kutangaza hatua yake ya kumfungulia mashtaka rais wa nchi hiyo Fouad Masoum, kwa tuhuma za kukiuka katiba ya nchi hiyo, askari wengi wameshuhudiwa katika maeneo muhimu ya jiji la Baghdad.

Duru kutoka jijini Baghdad zimearifu kuwa kwa hali isiokuwa ya kawaida, askari wengi wameonekana katika maeneo ya taasisi za serikali huku barabara kadha za jiji zikifungwa, saa chache baada ya waziri mkuu, Nouri al Malik kutangaza ghafla kuwa anaenda kufunguwa mashartaka dhidi ya rais.

Katika akaunti yake ya mtandao wa kijamii Twitter, serikali ya Marekani kupitia naibu waziri wa mambo ya nje anayehusika na maswala ya Iraq Brett McGurk, imesema itaendelea kumuunga mkono rais wa nchi hiyo Fouad Masoum, ambaye ndiye mlinzi halali wa taasisi za serikali pamoja na waziri mkuu ataye kubalika na pande zote.

Nouri al Malik kutoka jamii ya Mashia, ambaye alishinda uchaguzi mwezi April 30 mwaka huu na ambaye analenga kuwania muhula mwingine wa tatu, amekuwa akikosolewa sana na sera yake ambayo wengi wanasema ni ya kibaguzi dhidi ya watu wa chache wa jamii ya wa Sunni.

Bunge la taifa nchini humo ambalo lilitakiwa kukutana jana kujadili kuhusu swala la kupatikana kwa waziri mkuu anaye kubalika na pande zote, imeahirisha kikao chake hadi Agosti 19 baada ya kutotimia kwa idadi.

Wakati huo huo majeshi ya kikurdi kaskazini mwa Iraq yamesema limefanikiwa kudhibiti miji mingine miwili ya Wair na Maknur iliyokuwa inadhibitiwa na waasi wa ISIl.

Miji hiyo miwili imetekwa baada ya jeshi la Marekani kushambulia ngome za waasi hao wa Isil. Wakurdi wameapa kuendelea na mapiano hadi wahakikishe wameyakomboa maeneo yanayodhibitiwa na waasi iwapo watapatishiwa msaada wa kijeshi.

Kauli hiyo waliitamka jana jumapili wakati walipokuatana kwa mazungumzo na waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Laurent Fabius. Waziri huyo wa Ufaransa ameahidi kuwasilisaha maombi hayo mbele ya Umoja wa Ulaya.

Hayo yakijiri, misaada ya kiutu kutoka Ufaransa imewasili jana jumapili katika maeneo walikokimbilia jamii ya watu walio wachache wakihofia usalama wao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.