Pata taarifa kuu
CHINA-TAIWAN-JINPING-SIASA

China yasema ni lazima Taiwan ikubali kuwa haiwezi kuwa huru

Rais wa China Xi Jinping amewataka watu wanaoishi katika kisiwa cha Taiwan wakubali na lazima wafahamu kuwa Taiwan itaunganishwa na ni sehemu ya China.

Rais wa China Xi Jinping
Rais wa China Xi Jinping AFP/POOL/Mark Schiefelbein
Matangazo ya kibiashara

Jinping ametoa kauli hiyo, wakati wa maadhimisho ya miaka 40, tangu kuanza kuimarika kwa uhusiano kati ya Beijing na Taipei.

Kiongozi huyo wa taifa lenye watu wengi duniani, amesisitiza kuwa, China imekuwa ikijaribu kuhakikisha hilo linafanyika kwa amani lakini nguvu ya kijeshi itatumika iwapo kutakuwa na ulazima wa kufanya hivyo.

Taiwan ambayo inajitawala na ina rais wake, hata hivyo haijawahi kutangaza uhuru wa kujitenga na China.

Kiongozi wa nchi hiyo amesisitiza kuwa China na Taiwan ni familia moja ambayo inaunganishwa na historia moja na hivyo haiwezi kutenganishwa.

“Watu wa Taiwan lazima waelewe kuwa, Uhuru wao utawaletea matatizo,” amesema rais Jinping.

Ameonya kuwa Beijing, haiwezi kukubali uhuru wa Taiwan, ambao amesema unachochewa na nchi za kigani.

Uongozi wa kisiwa hicho, umeendelea kusisitiza kuwa hautishwi kauli za China kwa sababu kisiwa hicho kimepiga hatua ya kidemokrasia na inajisimamia.

China nayo imekuwa ikitishia kusitisha msaada wa kifedha hasa kwa mataifa ya Afrika, iwapo hayatasitisha uhusiano wao wa kidiplomasia na Taiwan.

Burkina Faso na Gambia ni miongoni mwa mataifa ambayo hivi karibuni yamevunja uhusiano na Taipei.

Taiwan ina idadi ya watu zaidi ya Milioni 23, makao makuu ya kisiwa hicho ni Taipei na inaongozwa na Tsai Ing-wen rais wa  kwanza mwanamke kushika madaraka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.