Pata taarifa kuu
UTURUKI-WAHAMAIJI-USALAMA

Saba wakufa maji baada ya boti kuzama nchini Uturuki

Watu saba wamefariki dunia na 64 wameokolewa wakati boti iliyobeba wahamiaji wa Pakistani, Bangladeshi na Afghanistan ilipozama katika Ziwa Van nchini Uturuki leo Alhamisi, viongozi wa eneo hilo wamesema.

Wahamiaji waendelea kukumbwa na mikasa mbalimbali baharini wanapojaribu kuingia Ulaya.
Wahamiaji waendelea kukumbwa na mikasa mbalimbali baharini wanapojaribu kuingia Ulaya. REUTERS/Guglielmo Mangiapane
Matangazo ya kibiashara

Ajali hiyo imetokea saa 03:00 saa za Uturuki (sawa na saa 00:00 usiku sa za kimataifa) karibu na pwani ya kaskazini ya ziwa Van, imesema ofisi ya gavana wa mkoa wa Bitlis katika taarifa.

Ziwa liko liko karibu na mpaka na Iran na ni eneo ambalo wahamiaji wengi wanatumia kwa kuingia Ulaya Magharibi.

Miili mitano imepatikana katika eneo la ajali na watu wengine wawili wamefariki dunia baada ya kufikishwa hospitalini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.