Pata taarifa kuu
CHINA-USHIRIKIANO

Rais wa China Xi Jinping ataka muungano wa China na Taiwan

Rais wa China Xi Jinping amesema jitihadi za kuungana na Taiwan, ni lazima, zitimie, wakati huu mvutano ukiendelea kati ya pande hizo mbili.

Rais Xi ametoa wito huo ikiwa ni siku kadhaa baada ya jeshi la China kutuma idadi kubwa ya ndege za kijeshi zilizokuwa zikiruka kuelekea Taiwan katika mazoezi ya kijeshi kitendo ambacho kisiwa hicho kimekiita kuwa ni tishio.
Rais Xi ametoa wito huo ikiwa ni siku kadhaa baada ya jeshi la China kutuma idadi kubwa ya ndege za kijeshi zilizokuwa zikiruka kuelekea Taiwan katika mazoezi ya kijeshi kitendo ambacho kisiwa hicho kimekiita kuwa ni tishio. Noel Celis AFP
Matangazo ya kibiashara

Xi amesema kuungana na Taiwan ni lazima ifanyike kwa amani, lakini hakueleza iwapo nguvu itatumiwa huku akisisitiza kuwa, masuala yake na Taiwan ni masuala ya ndani.

Kauli ya China hata hivyo, imemshtumiwa na Taiwan ambayo inasema hatima ya kisiwa hicho ipo mikononi mwa watu wake. Taiwan inasema inajitawala yenyewe lakini China inasema kisiwa hicho ni sehemu yake.

Kwa upande mwengine Waziri wa ulinzi wa Taiwan amesema mvutano wao na China umekuwa mbaya zaidi katika miaka 40 iliyopita.

China na Taiwan zilitengana mwaka 1949 wakati wa vita ya wenyewe kwa wenyewe, na chama tawala cha kizalendo cha wakati huo kilikimbilia katika visiwa hivyo na kumpa nafasi mkomunisti Mao Zedong kunyakua madaraka upande wa bara.

Mwaka huu Taiwan itafanya maonesho ya vifaa vya kijeshi ambayo ni nadra kufanyika na miongoni mwa vifaa hivyo ni makombora ya kivita. Jeshi la anga linatarajiwa pia kuonesha ndege za kivita. Maonesho hayo ya kijeshi yatafanyika katika madhimisho ya kitaifa Jumapili mbele ya jengo la ofisi ya Rais katikati mwa mji mkuu, Taipei.  

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.