Pata taarifa kuu

Zaidi ya watu 100 wamekufa nchini India na Nepal katika mafuriko na maporomoko ya ardhi

Zaidi ya watu 100 wamefariki dunia baada ya siku kashaa za mafuriko makubwa na maporomoko ya ardhi yaliyoharibu barabara na nyumba nchini India na Nepal, viongozi wamesema leo Jumatano, na kuengeza kuwa watu wengi hawajulikani waliko.

Maelfu ya watu walihamishwa na angalau kambi 100 zilitengwa kwa minajili ya kuwapa hifadhi, mkuu wa serikali ya Kerala Pinarayi Vijayan alisema Jumapili.
Maelfu ya watu walihamishwa na angalau kambi 100 zilitengwa kwa minajili ya kuwapa hifadhi, mkuu wa serikali ya Kerala Pinarayi Vijayan alisema Jumapili. REUTERS - REUTERS TV
Matangazo ya kibiashara

Jumatano hii idadi rasmi imeongezeka nchini India hadi watu 85 waliofariki dunia na 11 hawajulikani waliko na nchini Nepal idadi ya vifo imeongezeka hadi 31na 43 hawajulikani waliko.

Mamlaka ya hali ya hewa nchini India imeongeza muda wa tahadhari yao Jumanne wiki hii na kutabiri kuwa mvua kubwa zitanyesha katika ukanda huo kwa siku mbili zijazo.

Katika eneo la Uttarakhand kaskazini mwa India, viongozi wamesema watu 46 walifariki dunia katika siku za hivi karibuni na 11 hawajulikani waliko. Katika jimbo la pwani la Kerala (Kusini), mkuu wa serikali katika jimbo hilo, Pinarayi Vijayan, amebaini kwamba idadi ya vifo ni 39.

Karibu wahanga 30 huko Uttarakhand walipoteza maisha mapema Jumanne katika visa saba tofauti katika mkoa wa Nainital ulioathiriwa vibaya baada ya maporomoko ya ardhi na kuharibiwa kwa miundombinu, hali ambayo ilisababishwa na mafuriko makubwa.

Watu watano wa familia moja walifukiwa katika nyumba yao, amesema afisa wa eneo hilo, Pradeep Jain.

Waathiriwa wengine watano waliuawa katika maporomoko ya ardhi yaliyotokea wilayani Almora, kaskazini mwa Uttarakhand, na nyumba yao kuzama chini ya mawe na matope.

Kwa sababu ya maonyo ya hali ya hewa, mamlaka imeamuru shule zifungwe na kupiga marufuku shughuli zote za kidini au za watalii katika jimbo hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.