Pata taarifa kuu

Muungano wa Indo-Pacific: baada ya Korea Kusini, Joe Biden atarajiwa Japani

Rais wa Marekani Joe Biden anawasili Tokyo Jumapili hii baada ya kukaa zaidi ya siku mbili nchini Korea Kusini ili kuthibitisha ahadi ya Marekani ya kumtetea mshirika wake wa Korea Kusini dhidi ya Korea Kaskazini na kusisitiza haja ya kudumisha "huru na wazi" wa ukanda wa Indo-Pacific.

Jumapili, Mei 22, 2022, Rais wa Marekani Joe Biden anazuru Kambi ya kikosi cha jeshi la anga cha Osan huko Pyeongtaek. Wakati wa mchana, ataendelea na ziara yake ya Asia huko Japani.
Jumapili, Mei 22, 2022, Rais wa Marekani Joe Biden anazuru Kambi ya kikosi cha jeshi la anga cha Osan huko Pyeongtaek. Wakati wa mchana, ataendelea na ziara yake ya Asia huko Japani. REUTERS - JONATHAN ERNST
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Marekani anakuja Tokyo kushiriki katika mkutano wa kilele wa Quad siku ya Jumanne, unaoleta pamoja Marekani, Japan, India na Australia.

Kwa mujibu wa Rais Joe Biden, muungano wa Quad lazima usaidie kuzuia kujiimaisha kwa China katika eneo la Indo-Pasifiki, ikizingatiwa hatari ya uvamizi wa China kwa Taiwan na kuongezeka kwa luteka za kijeshi kati ya China na Urusi katika ukanda huo.

Huko Tokyo, muungano huu usio rasmi utaongeza programu ya kiuchumi kwenye mfumo wake wa usalama kwa sababu ya matatizo na India kuhusu masuala ya ulinzi. Marekani itazindua kundi jipya la kiuchumi, lililo wazi kwa nchi za eneo la Indo-Pasifiki, linalonuiwa kuunganisha mazingira, biashara, viwango vya kidijitali na kuanzisha mfumo wa ugavi bila China.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.