Pata taarifa kuu

Nepal yatoa wito kwa India kuacha kusajili raia wake katika jeshi lake

Zaidi ya Wanepali 1,000 wanasemekana kujiunga na jeshi la India hivi majuzi chini ya mpango tata wa kuajiri wanajeshi wapya, Agneepath. Nepal inahofia kwamba wale ambao watafeli mafunzo haya mapya watarejea katika nchi zenye vurugu zaidi.

Tangu makubaliano ya 1947, jeshi la India limekuwa likiajiri wanajeshi wapya kutoka nchini Nepal.
Tangu makubaliano ya 1947, jeshi la India limekuwa likiajiri wanajeshi wapya kutoka nchini Nepal. REUTERS/Mukesh Gupta/Files
Matangazo ya kibiashara

Chini ya makubaliano ya 1947 majeshi ya India yameweza kuajiri wanajeshi kutoka Nepal kwa miaka 75 iliyopita. Kathmandu pia ni mshirika wa kihistoria wa New Delhi katika Himalaya. Lakini mpango mpya wa jeshi la India wa kuajiri wanajeshi wapya, uliopewa jina la Agneepath, "njia ya moto", unaonekana kusababisha utata katika nchi hizo mbili.

Robo tatu ya watu walioshindwa mafunzo ya kijeshi

Inatoa muda wa miaka minne katika jeshi baada ya hapo ni 25% tu ya wanajeshi watajumuishwa katika vikosi vya kudumu. Mnamo mwezi wa Juni, hali hii ilichochea hasira iliyoenea kati ya wanafunzi na baadhi ya wanasiasa wa India ambao wanaona kama upotoshaji wa hadhi ya wafanyakazi wa serikali na vikosi vya jeshi.

"Tuna wasiwasi sana kuhusu mustakabali wa asilimia 75 ya waajiriwa ambao watapoteza kazi zao baada ya kufunzwa," amesema Narayan Khadka, Waziri wa Mambo ya Nje wa Nepali. Vijana kama hao ambao wamebaki bila kazi na mafunzo ya mapigano ya kijeshi wanaweza kuzua vurugu nchini. »

Mafunzo yasitishwa

Alhamisi hii, Nepal ilisitisha mafunzo ya raia 1,300 ambao walijiandikisha kwa mpango huu. Takriban Wanepali 35,000 kwa sasa wanaaminika kuwa wanajeshi wa jeshi la India.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.