Pata taarifa kuu
NEPAL -AJALI

Watu 67 wafariki katika ajali ya ndege Nepal

Watu 67 ndio wamethibitishwa hadi sasa kuwa wamefariki baada ya ndege iliyokuwa na abiria 72 kuanguka nchini Nepal, polisi nchini humo wamethibitisha.

Ajali ya ndege Nepal
Ajali ya ndege Nepal © via REUTERS / HANDOUT
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa mamlaka ya anga nchini Nepal, hii ni ajali mbaya zaidi kuwahi kutokea kwenye taifa hilo katika kipindi cha karibu miongo mitatu.

Polisi nchini humo wamethibitisha kupata miili zaidi ya 50 huku wakisema wanajaribu kutoa miili mingine iliyoko kwenye bonde lililo na urefu wa mita 300, ambapo ndege hiyo iliangukia, vikosi vya uokozi vikiwa havina matumaini ya kupata abiria yeyote aliyenusurika.

Msemaji wa polisi Krishna Prasad, amesema zoezi la uokoaji limekuwa gumu kutokana na sehemu ambayo ndege hiyo imeangukia.

Mamlaka zimesema miongoni mwa abiria waliokuwemo kwenye ndege hiyo ni raia wa kigeni kutoka nchi za India, Urusi na Korea.

Ndege hiyo aina ya ATR 72, ilianguka muda mfupi baada ya kuruka kutoka kwenye uwanja wa Kathmandu ikielekea Pokhara, ambapo iligonga mwamba na kuanguka katika bonde.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.