Pata taarifa kuu
NEPAL- AJALI YA NDEGE

Ajali ya ndege Nepal: Shughuli ya kutafuta miili inaendelea

Wafanyakazi wa uokoaji nchini Nepal, wanaendelea na zoezi la kutafuta miili ya watu wanne ambao hawajapatikana baada ya ajali ya ndege iliyokuwa na abiria 72, mamlaka zikisema hakuna matumaini ya kupata walio hai.

У Непалі розбився пасажирський літак
У Непалі розбився пасажирський літак © via REUTERS / HANDOUT
Matangazo ya kibiashara

Hadi sasa miili ya watu 68 ilikuwa imepatikana kati ya watu 72 walioorodheshwa kusafiri na ndege hiyo aina ya ATR 72 ya shirika Yeti.

Wafanyakazi wa uokoaji tangu jana walikuwa wakijaribu kukabiliana na hali mbaya ya hewa katika eneo ambako ndege hiyo ilianguka, wataalamu wakisema zoezi limekuwa gulu kutokana na ukubwa wa bonde lenye karibu mita 300.

Kwa siku ya pili wanajeshi na wafanyakazi wengine, walikuwa wakiendelea kukusanya mabaki ya ndege hiyo, iliyokuwa itumie dakika 27 pekee kutoka Kathmandu hadi kwenye mji wa Pokhara.

Kiongozi wa operesheni za uokoaji kwenye eneo la tukio, amesema wataendelea kuitafuta miili iliyosalia, huku maiti zilizopatikana zitafanyiwa uchunguzi wa kisayasi kwa utambuzi kabla ya kukabidhiwa kwa familia zao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.