Pata taarifa kuu
NEPAL- AJALI YA NDEGE

Raia wa Nepal wanaomboleza vifo vya watu 67 baada ya ajali ya ndege

Raia wa Nepal wanaomboleza baada ya kuanguka kwa ndge ya abiria na kuwauwa watu 67, ikiwa ni ajali mbaaya kuwahi kutokea nchini humo kwa kipindi cha miaka 30.Serikali ya Nepal imetangaza uchunguzi kubaini chanzo cha ajali hiyo.

Ajali ya ndege nchini Nepal
Ajali ya ndege nchini Nepal AP - Krishna Mani Baral
Matangazo ya kibiashara

Ajali hiyo ilitokea jana, wakati ndege hiyo ilipokuwa imetoka mji wa Kathmandu kwenda katika mji wa kitalii wa Pokhara.

Mikanda ya vídeo inayosambaa, iliyochukuliwa na simu, inaonesha ndege hiyo ya Shirika la ndege la Yeti, ikianguka kutoka angani, wakati ikikaribia kutua kwenye uwanja ndege.

Shughuli za kutafuta miili ya abiria iliyositishwa jana  kwa sababu ya giza, inarejelewa asubuhi hii, ikiiongozwa na mamia ya wanajeshi wa Nepal.

Mpaka sasa, hiajafahamika chanzo cha ajali hiyo, wakati huu serikali ikitangaza uchunguzi kubaini kuaguka kwa ndege hiyo.

Nchi ya Nepal, ina historia mbaya ya kushuhudia kwa ajali kama hizi, kutokana na kile kinachoelezwa kuwa na miundo mbinu mibaya, ikiwa viwanja vingo vya ndege kuzungukwa kwa milima.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.