Pata taarifa kuu
USHIRIKIANO-DIPLOMASIA

Blinken nchini China: Washington yakaribisha majadiliano 'ya uaminifu', Beijing yapongeza

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken na Waziri wa Mambo ya Nje wa China Qin Gang walikubaliana Jumapili Juni 18 mjini Beijing kuleta utulivu kati ya mataifa hayo mawili yenye nguvu kiuchumi duniani. Ziara ya Blinken ni ya kwanza kufanywa na waziri wa mambo ya nje wa Marekani nchini China tangu mwezi Oktoba 2018.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken (katikati) akiambatana na Waziri wa Mambo ya Nje wa China Qin Gang (kulia), mjini Beijing Juni 18, 2023.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken (katikati) akiambatana na Waziri wa Mambo ya Nje wa China Qin Gang (kulia), mjini Beijing Juni 18, 2023. AFP - LEAH MILLIS
Matangazo ya kibiashara

Katika siku ya kwanza ya ziara ya Waziri wa Mambo ya Nje Antony Blinken mjini Beijing ili kupunguza mvutano, Marekani ilipongeza majadiliano "ya kujenga" na "ya ukweli" siku ya Jumapili, na kukaribisha makubaliano yaliyotolewa na mkuu wa diplomasia ya China katika ziara ijayo ya Washington.

Wawili hao walikuwa na mazungumzo "ya ukweli, muhimu, na ya kujenga," msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje Matthew Miller alisema baada ya mkutano huo. Antony Blinken alisisitiza hasa "umuhimu wa diplomasia na kudumisha njia wazi za mawasiliano katika masuala yote ili kupunguza hatari ya dhana potofu na hesabu zisizo sahihi", alisema.

Antony Blinken pia alimwalika Qin Gang. Waawili hao walikubaliana "kupanga ziara kama hiyo kwa tarehe inayofaa kwa pande zote," ambayo itaamuliwa baadaye, kulingana na msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani Matt Miller.

"Leo nilikutana na mshauri wa serikali na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Watu wa China Qin Gang huko Beijing na kujadili jinsi tunaweza kusimamia kwa uwajibikaji uhusiano kati ya nchi zetu mbili kupitia njia za mawasiliano wazi," Blinken ameandika kwenye Twitter.

"Mahusiano katika kiwango cha chini kabisa"

Kwa upande wake, Waziri wa Mambo ya Nje wa China alimkumbusha mwenzake wa Marekani kwamba uhusiano kati ya Beijing na Washington yalikuwa "katika kiwango cha chini kabisa" tangu mwanzo wa kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili mwaka 1979, kulingana na maoni yaliyoripotiwa na televisheni ya serikali, CCTV.

Bw. Qin “alisisitiza kuwa uhusiano kati ya China na Marekani uko chini kabisa tangu kuanzishwa kwake. Haijalishi masilahi ya kimsingi ya watu hao wawili na haifikii matarajio ya pamoja ya jumuiya ya kimataifa," msaidizi wa Waziri wa Mambo ya Nje wa China Hua Chunying ameandika kwenye Twitter.

Miongoni mwa mambo ya kuzingatia, mkuu wa diplomasia ya China alisema kuwa Taiwan ndiyo nyeti zaidi.

"Suala la Taiwan ni suala la msingi la maslahi makubwa ya China, suala muhimu zaidi katika uhusiano wa China na Marekani na hatari kubwa zaidi kwao," Qin Gang alisema.

Ziara ya mkuu wa diplomasia ya Marekani ilipangwa awali mwezi Februari, kufuatia mkutano, mwezi Novemba mwaka jana, kati ya rais wa Marekani Joe Biden na mwenzake wa China Xi Jinping, kando ya mkutano wa kilele wa G20 nchini Indonesia. Lakini ulifutwa dakika za mwisho kufuatia mvvutano baada ya China kurusha puto juu ya anga ya Marekani, ambayo ilisema kuwa  puto hilo nindege ya "kijasusi", wakati Beijing ilihakikisha kwamba ilikuwa chombo cha hali ya hewa kilichotoka kwenye njia yake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.