Pata taarifa kuu

Watu sita wamefariki katika ajali ya helikopta nchini Nepal

Nairobi – Abiria wote sita waliokuwa wameabiri ndege ya watali aina ya helikopta nchini Nepal, wamefariki baada ya ndege hiyo kuanguka muda mfupi baada ya kupaa karibu na mlima Everest, mamlaka ya usafiri wa anga nchini humo imethibitisha.

 Ajali za ndege zimekuwa zikiripotiwa katika mlima Evereste
Ajali za ndege zimekuwa zikiripotiwa katika mlima Evereste REUTERS - Monika Deupala
Matangazo ya kibiashara

Helikopta hiyo inayomilikiwa na kampuni ya Manang Air, ilikuwa ikielekea katika jiji kuu la Kathmandu ikitokea kwenye eneo la Lukla kwa ajili ya shughuli za kitali kabla ya kupoteza mawasiliano dakika kumi baadae baada ya kupaa.

Kwa mujibu wa Gyanendra Bhul, afisa kutoka mamlaka ya usafiri wa anga nchini humo, miili ya sita hao imepatikana katika eneo la ajali.

Nepal inafahamika kutokana na kutokuwa na hakikisho la usalama wa angani ,tukio hili la hivi punde likitokea miezi sita baada ya ajali nyengine ya ndege kuwaua watu wote 72 waliokuwa wameiabiri ndege magaharibi mwa taifa hilo.

Wataalam wa usafiri wa anga wanaeleza kuwa taifa hilo linakabiliwa na idadi kubwa ya ajali za ndege kutokana na uwepo barafu nchini humo, hali ambayo imekuwa mojawapo wa changamoto zinazowakabili marubani.

Kando na changamoto ya barafu, sekta ya anga nchini Nepal inakabiliwa na uhaba wa mafunzo kwa marubani pamoja na ukosefu wa mipango bora ya kutekeleza marekebisho katika maeneo yanayohitajika.

Tume ya Ulaya imepiga mafaruku ndege kutoka kwa taifa hilo kutumia anga yake kutokana na masuala ya kiusalama.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.