Pata taarifa kuu

India: Mvua kubwa yasababisha vifo vya watu 49

Mafuriko makubwa yaliyodumu siku kadhaa na maporomoko ya udongo yamewaua watu 49, ikiwa ni pamoja na 9 katika mkasa wa kuporomoka kwa hekalu.

Sehemu ya jengo liliporomoka siku ya Jumatatu kando ya Mto Maldevta katika jimbo la Uttarakhand baada ya mvua kubwa kunyesha.
Sehemu ya jengo liliporomoka siku ya Jumatatu kando ya Mto Maldevta katika jimbo la Uttarakhand baada ya mvua kubwa kunyesha. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Mvua kubwa zilizonyesha kwa siku kadhaa zimeharibu madaraja na majengo, na kusomba magari katika majimbo ya kaskazini ya Uttarakhand na Himachal Pradesh.

Katika jimbo la Himachal Pradesh, watu 41 wamefariki katika muda wa saa 24 zilizopita, Waziri Mkuu wa jimbo hilo Sukhvinder Singh Sukhu amesema, wakiwemo 9 katika mkasa wa kuporomoka kwa hekalu la Kihindu katika mji mkuu wa jimbo hili, Shimla.

"Utawala wa eneo hilo unafanya kazi ya kusondoa uchafu na mabaki ya majengo ili kuokoa watu ambao wanaweza kuwa wamenaswa," waziri mkuu amesema katika taarifa.

Rais wa India, Droupadi Murmu, amesema "ameumizwa na watu kupoteza maisha katika tukio hilo kubwa linalohusiswa na mvua". Drupadi Murmu pia ametoa rambirambi zake kwa familia katika jimbo lililoathiriwa zaidi la Himachal Pradesh.

Katika maeneo yaliyoathiriwa zaidi, barabara kuu na njia za umeme zimeharibiwa vibaya, na kuwazuia maelfu ya watu. Njia ya reli pia ilipata uharibifu mkubwa.

Mafuriko yanaongezeka na mabadiliko ya hali ya hewa

Katika jimbo jirani la Uttarakhand, makundi ya waokoaji yamejaribu kuwaondoa watu waliofukiwa kufuatia maporomoko ya udongo yaliyosababishwa na mvua kubwa.

Karibu na kingo za Ganges, katika mji wa kitalii wa Rishikesh, ulioko Uttarakhand, watu watano walijikuta wamenasa chini ya vifusi kufuatia maporomoko ya udongo.

Miongoni mwao, ni msichana mdogo tu aliyeokolewa, amesema kamishna wa polisi wa wilaya, na kuongeza kuwa familia yake yote bado imenaswa chini ya vifusi. Kwa jumla, takriban watu wanane wamefariki tangu Ijumaa katika jimbo hili, kulingana na mamlaka.

Sukhvinder Singh Sukhu ametoa wito kwa wakaazi wa jimbo la Himachal Pradesh kukaa nyumbani na kuepuka kwenda karibu na mito. Shule katika jimbo hilo zimefungwa, ameongeza.

Mvua za masika huchangia takriban 80% ya mvua kwa mwaka huko Asia Kusini. Ni muhimu kwa viwango vya mito, kujaza maji ya ardhini na kilimo. Lakini pia husababisha vifo na uharibifu unaosababishwa na mafuriko na maporomoko ya udongo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.