Pata taarifa kuu

India yarusha roketi yake juani baada ya mwezini kufanikiwa

NAIROBI – India imezindua misheni nyingine juani Jumamosi, wiki moja baada ya misheni ya mwezini kufaulu.

Chombo cha anga cha Aditya-L1 kikipaa kutoka kituo cha anga za juu huko Sriharikota, India, Jumamosi, Septemba 2, 2023.
Chombo cha anga cha Aditya-L1 kikipaa kutoka kituo cha anga za juu huko Sriharikota, India, Jumamosi, Septemba 2, 2023. AP
Matangazo ya kibiashara

Chombo cha Aditya-L1, kimezinduliwa muda mfupi kabla ya saa sita mchana, na shughuli hiyo kutangazwa moja kwa moja ikionyesha mamia ya watazamaji wakishangilia.

Chombo hiki kimebeba vifaa vya kisayansi vitakavyotumika kutazama jua katika misheni hii ya miezi minne.

Uzinduzi umefanikiwa, na mambo yameenda vizuri, alitangaza afisa wa Shirika la Utafiti wa Anga la India kutoka kwa kituo cha misheni wakati chombo hicho kikielekea kwenye sehemu za juu za angahewa ya dunia.

 

Iwapo misheni hii ya hivi punde zaidi kutoka kwa Shirika la Utafiti wa Anga la India (ISRO) itafaulu, basi itakuwa ya kwanza kwa taifa lolote la Asia kuwekwa kwenye obiti kuzunguka Jua.

 

Misheni hi pia inalenga kutoa mwanga juu ya mienendo ya matukio mengine kadhaa ya jua kwa kupiga picha na kupima chembe katika anga ya juu ya Jua.

Nchi ya Marekani na Shirika la Anga za Juu la Ulaya (ESA) wametuma uchunguzi mwingi katikati ya mfumo wa jua, kuanzia na mpango wa pioneer wa NASA katika miaka ya 1960.

Kadhalika Japan na China pia zimezindua misheni zao za uchunguzi wa jua kwenye mzunguko wa Dunia.

India pia inapanga misheni ya pamoja na Japan kutuma uchunguzi mwingine kwa Mwezi kufikia 2025 na misheni ya obiti kwa Zuhura ndani ya miaka miwili ijayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.